Bhisumbinyama
JF-Expert Member
- Dec 26, 2019
- 797
- 581
Kangi hoyeeee! Huyu jamaa alijishaua sana. Acha ahojiwe ikiwezekana afungwe kabisa.Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola aitwa na TAKUKURU kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma za kuingia mkataba wa kimangungo wa zaidi ya Shilingi Trillioni moja.
Kumbe nawewe kuna yanayokuumizaMungu kajibu maombi ya walokole alikuwa akiwanyanyasa tulimuonya humu.Lugora kaa mbali na kunyanyasa walokole akajitia kichwa ngumu yako wapi? Akaingia kunyanyasa mitume na manabii hadharani kilichomkuta halali yake.Nakala imfikie Sophia Mjema na mkurugenzi wa mji wa Babati .Lugora ananyolewa wao watie maji
Utaanza wewe kwanza!
Na wewe unaamini kuwa kuna chochote kitafanyika? Kule atafika na kunywa juice tu, mbona mawaziri kibao wameshatumbuliwa na hawashtakiwi!!!Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola aitwa na TAKUKURU kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma za kuingia mkataba wa kimangungo wa zaidi ya Shilingi Trillioni moja.
Media hazina akili sawasawa ni kama zimekufa ganziVyombo vyote vya dola pamoja na media zinamshukia Lugola kama mwewe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati mwingine unaweza kupata kazi sana kum-support Jiwe,anafanya mambo kinyumenyume sana mpaka unashindwa kuelewa nia yake hasa katika haya mambo ya rushwa ipo wapi??Maana tukumbuke huyu mtu naye atatoka madarakani,na nchi yetu itabaki.Ina miaka mitano tu mbele...maana ni hakika kwa mfumo wetu,huo mwezi October atashinda tu.
Huyu Kangi Lugola hakupaswa kabisa kuwepo kwenye hilo baraza na hii Wizara,huyu na Mwambalaswa na yule Mbunge wa Morogoro Mvomelo,walikutwa na shutuma za rushwa,kesi ikaisha kiajabu ajabu ili kutokukichafua chama,huyohuyo Lugola tena unampa wizara unategemea nini??
Halafu kwa sasa,ili kiongozi wa Serikali asafiri nje ya nchi,ni lazima awe na kibari cha Kutoka Msajili wa Hazina na Ikulu.Msajili wa Hazina anajiridhisha kuwa safari hiyo ina manufaa kwa nchi na haitaigharimu serikali pesa nyingi,kama safari inahusisha nauli,per diem n.k toka serikalini,msajili lazima ajiridhishe kuwa jambo hilo lina manufaa kwa nchi.
Hawa wa ngazi za kina Kangi Lugola,Katibu Mkuu na wengine wenye uteuzi wa ki-Rais,Mzee lazima ajue wanatoka nje ya nchi.Kwa wizara kama ya Mambo ya ndani ambayo ni ya Kiulinzi,Waziri kila siku kabla hajalala lazima afikishe report ya mambo ya usalama wa raia na nchi.Sasa kama alienda safari zote huko Romania huyu Jiwe hakujua??Yaani mpaka unasainiwa mkataba yeye hakuwa na taarifa??
Kama hakuwa anajua lolote,basi hapa tatizo kubwa ni Jiwe na hawa kina Kangi na Andengenye ni "bangusilo" tu.
Inashangaza sana.Ile hotuba ya Rais mwenye vyombo vyote anaishia kulalamika,analialia mbele ya Raia...Mzee kama Rais unatakiwa usilielie,toa suluhisho,ukiona wizara inakutesa ujue wewe pia umeshindwa?Inaposhindwa Wizara ujue na Rais kashindwa...Hii ndio dhana ya "Collective Responsibility"
Aende tu,na isiishie kwenye mahojiano tu, aswekwe ndani na atemeshwe hela yetu,we are fed up with these people.Kwanza sioni hata mantiki ya mahojiano,ushahidi wote si upo?Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola aitwa na TAKUKURU kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma za kuingia mkataba wa kimangungo wa zaidi ya Shilingi Trillioni moja.
We MaMa kimekukuta nini..!?Ilikuwaje Magufuli akamteua mtu aliewahi shitakiwa kwa kula Rushwa ? Ila Magufuli nae anatuangusha sana.
Mungu kajibu maombi ya walokole alikuwa akiwanyanyasa tulimuonya humu.Lugora kaa mbali na kunyanyasa walokole akajitia kichwa ngumu yako wapi? Akaingia kunyanyasa mitume na manabii hadharani kilichomkuta halali yake.Nakala imfikie Sophia Mjema na mkurugenzi wa mji wa Babati .Lugora ananyolewa wao watie maji
Kwajinsi alivyo nona mgongoni....
Ukijibiwa usinisahauNaomba kujuzwa: Hivi mikataba ya kimataifa wizara husika inaweza kuingia bila kuidhinishwa na Mwanasheria Mkuu wa serikali??
Sent using Jamii Forums mobile app
Mwongo mwogoze.Sasa kama alienda safari zote huko Romania huyu Jiwe hakujua??Yaani mpaka unasainiwa mkataba yeye hakuwa na taarifa??