Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola adaiwa kuwa chini ya ulinzi

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola adaiwa kuwa chini ya ulinzi

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola aitwa na TAKUKURU kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma za kuingia mkataba wa kimangungo wa zaidi ya Shilingi Trillioni moja.
Kangi hoyeeee! Huyu jamaa alijishaua sana. Acha ahojiwe ikiwezekana afungwe kabisa.
 
Mungu kajibu maombi ya walokole alikuwa akiwanyanyasa tulimuonya humu.Lugora kaa mbali na kunyanyasa walokole akajitia kichwa ngumu yako wapi? Akaingia kunyanyasa mitume na manabii hadharani kilichomkuta halali yake.Nakala imfikie Sophia Mjema na mkurugenzi wa mji wa Babati .Lugora ananyolewa wao watie maji
Kumbe nawewe kuna yanayokuumiza
 
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola aitwa na TAKUKURU kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma za kuingia mkataba wa kimangungo wa zaidi ya Shilingi Trillioni moja.
Na wewe unaamini kuwa kuna chochote kitafanyika? Kule atafika na kunywa juice tu, mbona mawaziri kibao wameshatumbuliwa na hawashtakiwi!!!
 
Kuna wengi tu walipashwa kuburuzwa mahakamani kama akina George Simbachawene, Charles Kitwanga, Medard Kalemani, Kafumu, Makonda na wengine wengi lkn kwa kuwa double standard ndio sera, bado wako salama.

Hatuambiwi ni kwa nini manunuzi mengi tu tena ya hela nyingi yanafanyikia ikulu bila hata bunge kuidhinisha na hatujui ni kwa vipi haya ndio yamevaliwa njuga kiasi hicho.
 
Wakati mwingine unaweza kupata kazi sana kum-support Jiwe,anafanya mambo kinyumenyume sana mpaka unashindwa kuelewa nia yake hasa katika haya mambo ya rushwa ipo wapi??Maana tukumbuke huyu mtu naye atatoka madarakani,na nchi yetu itabaki.Ina miaka mitano tu mbele...maana ni hakika kwa mfumo wetu,huo mwezi October atashinda tu.

Huyu Kangi Lugola hakupaswa kabisa kuwepo kwenye hilo baraza na hii Wizara,huyu na Mwambalaswa na yule Mbunge wa Morogoro Mvomelo,walikutwa na shutuma za rushwa,kesi ikaisha kiajabu ajabu ili kutokukichafua chama,huyohuyo Lugola tena unampa wizara unategemea nini??

Halafu kwa sasa,ili kiongozi wa Serikali asafiri nje ya nchi,ni lazima awe na kibari cha Kutoka Msajili wa Hazina na Ikulu.Msajili wa Hazina anajiridhisha kuwa safari hiyo ina manufaa kwa nchi na haitaigharimu serikali pesa nyingi,kama safari inahusisha nauli,per diem n.k toka serikalini,msajili lazima ajiridhishe kuwa jambo hilo lina manufaa kwa nchi.

Hawa wa ngazi za kina Kangi Lugola,Katibu Mkuu na wengine wenye uteuzi wa ki-Rais,Mzee lazima ajue wanatoka nje ya nchi.Kwa wizara kama ya Mambo ya ndani ambayo ni ya Kiulinzi,Waziri kila siku kabla hajalala lazima afikishe report ya mambo ya usalama wa raia na nchi.Sasa kama alienda safari zote huko Romania huyu Jiwe hakujua??Yaani mpaka unasainiwa mkataba yeye hakuwa na taarifa??

Kama hakuwa anajua lolote,basi hapa tatizo kubwa ni Jiwe na hawa kina Kangi na Andengenye ni "bangusilo" tu.

Inashangaza sana.Ile hotuba ya Rais mwenye vyombo vyote anaishia kulalamika,analialia mbele ya Raia...Mzee kama Rais unatakiwa usilielie,toa suluhisho,ukiona wizara inakutesa ujue wewe pia umeshindwa?Inaposhindwa Wizara ujue na Rais kashindwa...Hii ndio dhana ya "Collective Responsibility"

Kwani wewe mkeo akikuomba ruhusa anaenda kwenye party ukamruhusu akifanya mapenzi huko kosa linakuwa lako au la kwake? Na ukijua hutachukua hatua dhidi yake kwa kuwa ulimruhusu wewe mwenyewe? Tumia akiri, hata kama aliruhusiwa hakutakiwa kuandaa mikataba ya hovyo.
 
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola aitwa na TAKUKURU kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma za kuingia mkataba wa kimangungo wa zaidi ya Shilingi Trillioni moja.
Aende tu,na isiishie kwenye mahojiano tu, aswekwe ndani na atemeshwe hela yetu,we are fed up with these people.Kwanza sioni hata mantiki ya mahojiano,ushahidi wote si upo?
 
Ni kumpa pole tu .. Sidhani kama atachomoka hapa.
 
Wewe naye ni mlokole?
Mungu kajibu maombi ya walokole alikuwa akiwanyanyasa tulimuonya humu.Lugora kaa mbali na kunyanyasa walokole akajitia kichwa ngumu yako wapi? Akaingia kunyanyasa mitume na manabii hadharani kilichomkuta halali yake.Nakala imfikie Sophia Mjema na mkurugenzi wa mji wa Babati .Lugora ananyolewa wao watie maji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom