Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola adaiwa kuwa chini ya ulinzi

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola adaiwa kuwa chini ya ulinzi

Mtu aliywmewahi kuwa na mashitaka ya rushwa hakupaswa kuwa waziri in the first place.
Mteuaji hayupo makini au ana sababu zake binafsi za kufanya hivyo.
Nilishangaa sana Kangi kuteuliwa kuwa waziri. Hafai!
mteuaji bi binadamu kama ulivyo wewe na mimi
 
Kiuhalisia nchi ina mfumo mbovu sana hususani swala la mikataba hasa yenye maslahi mapana kitaifa
 
Mh Kangi, unatakiwa kuvaa kininja tena wakati unahojiwa na hao TAKUKURU!

 
Walisaini juu kwa juu......eti kwa niaba!
Inawezekana sisi Tanzania tukawa 'wajinga na wapuuzi' kufanya vitu kienyeji, itashangaza kama kampuni ya Romania nao watakuwa 'wajinga na wapuuzi' kufanya vitu kipuuzi na kukubali saini kutoka kwa watu wasio na mamlaka
 
Najitahidi niamini hiki kisa lakini moyo hautaki

Politics is when you say you are going to do one thing while intending to do another. Then you do neither what you said nor what you intended.
Saddam Hussein

 
Anatiwa leo kwenye hali hiyo, zamu ya wanaomuita ni kesho, na zamu yako ni kesho kutwa.

Tuweke akiba ya maneno
 
Upepo wa Pesa,
Mzee angalia kule, usiangalie kwenye vidole vya miguu yako. Hii issue inaonekana KAMA ni kubwa zaidi ya tunavyodhani, na sababu iliyotolewa ni kwa ajili yetu sisi raia, ila nadhani wenye mamlaka wanajua kitu tofauti. Nachelea kusema kuwa issue yenyewe inaweza hata isiwe inahusiana na mambo ya mkataba.

Ingekuwa mkataba hata Wizara ya Fedha kuna watu wangehusika. Kwani yulel Balozi aliwahi kurudishwa nyumbani na akanyang'anywa hadhi ya ubalozi sababu zake wewe uliwahi kujua ilikuwa nini? Inawezekana hata kwenye swala hili, sababu halisi hazijatajwa ila kosa lipo limefanyika, na laweza kuwa ni kubwa zaidi ya tunavyofikiria
 
Tanzania mtuhumiwa anabaki kuwa hana hatia mpaka itakapothibitishwa na mahakama kuwa ametenda kosa. Na huyu mheshimiwa ataendelea kuwa hana hatia mpaka mahakama itakapothibitisha vinginevyo. Naona wachangiaji wengi ni kama vile wameshahitimisha kuwa huyu mheshimiwa ana hatia.
 
The Sheriff,
Wanamuandama Kange tu kila siku mbona fisadi na mpiga dili mkuu hakamatwi au yeye yupo juu ya sheria?
 
Back
Top Bottom