Aliyemchoma Maduro kapata dola za kimarekani milion hamsini tasilimu, lakini...

Aliyemchoma Maduro kapata dola za kimarekani milion hamsini tasilimu, lakini...

Jana nchi ya Cuba imepokea masalia ya Walinzi maalum wa aliyekuwa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, nchi ya Cuba ilimpa Maduro jumla ya Walinzi 32 wenye mafunzo ya juu pamoja na vyeo vikubwa sana Jeshini akiwemo huyo pichani ambaye alikuwa anatambulika kama Kanali Humberto Alfonso Roco ambaye alikuwa Mkatoliki wa kweli mwenye mafunzo ya juu mpaka Kanisa Katoliki lilipa nafasi ya kumlinda Papa Francis anapotembelea Latin America kama hapo pichani lakini pia aliwahi kuongoza kikosi cha nje cha Ulinzi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry.

Inaelezwa kuwa Cuba imepoteza Wanajeshi wenye mafunzo ya juu mno wenye ngazi za Meja, Luteni na Makanali ambapo Manusura wa Oparesheni hiyo Marekani wanadai Delta Force wa Marekani walitumia mbinu ya hali juu mno sambamba na teknolojia ambayo hawakuwahi kuiona wala kuisikia ikitajwa pia kuna vitu kama mionzi iliyowapa Kikosi maumivu makali na waliuwa kwa haraka na muda mfupi kisha kuondoka na Maduro.
1768550213942.jpg
 
Back
Top Bottom