Watu mnatakiwa kujuwa,: ukisha mwaga damu ya binadamu mwezako, hata usipo kamatwa au kufahamika, azabu utakayo ipata ukiwa bado Hai ni kubwa kuliko uliye muuwaji. Kamwe usiuwe kwasababu yoyote ile. Ukiuwa maana yake na wewe uliye uwa unakuwa umeuwa nafusi yako mwenyewe kabla hujafa kimwili.View attachment 2859929
Mtuhumiwa anayedaiwa kusababisha kifo cha Beatrice Minja kwa kumchoma visu mara 25, Lucas Tarimo amafariki dunia akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi wakati akiendelea na matibabu katika hospitali ya Huruma iliyopo Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro.
Daktari kiongozi wa Hospitali ya Huruma wilayani hapa, Daria Mushi amethibitisha kutokea kwa kifo chake ambapo amesema amefariki jana Jumatatu, Januari Mosi, 2024 saa nne na nusu usiku.