Aliyemchoma Mwanamke visu 25 na kumsababisha Kifo afariki dunia akiwa chini ya ulinzi

Aliyemchoma Mwanamke visu 25 na kumsababisha Kifo afariki dunia akiwa chini ya ulinzi

View attachment 2859929
Mtuhumiwa anayedaiwa kusababisha kifo cha Beatrice Minja kwa kumchoma visu mara 25, Lucas Tarimo amafariki dunia akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi wakati akiendelea na matibabu katika hospitali ya Huruma iliyopo Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro.

Daktari kiongozi wa Hospitali ya Huruma wilayani hapa, Daria Mushi amethibitisha kutokea kwa kifo chake ambapo amesema amefariki jana Jumatatu, Januari Mosi, 2024 saa nne na nusu usiku.
akiendelea kupatiwa matitabu ya nini sasa, ya ugonjwa gani mbona hawafunguki? au ndio hiyo sumu waliyosema alijaribu kunywa ajiue.
 
Kama na yeye kajiuwa basi sio mbaya wameona wafe wote usiku
Tunawatakia safari njema ila nyie wachaga mungu anawaona jaman
 
Je, Amekufa kifo cha kawaida (natural death) au kuna mkono wa mtu??
Ni kwa nini siku zote hizo alikuwa bado yupo mahabusu ya Jeshi la Polisi badala ya kupekekwa katika Gereza la Mahabusu chini ya Jeshi la Magereza?????
Alikuwa bado hajakamatwa, ni baada ya wanaharakati wa mitandaoni kupiga kelele sana ndio akakamatwa.
 
kama mtu ashakutana na vijana wa hovyo kama hawa ataelewa kuna walakini sehemu kuna familia moja dada wa kijana huyo wa hovyo wana ukwasi na bahati kubwa serikalini na vyeo kedekede(wachaga jirani na huko rombo)kijana huyo wa hovyo majirani wameishia kumuogopa nakata watu masikio mara kabaka anafichwa kesi zinishia kwa majaji kwa rufaa mtuhumiwa anarudi tena kijijini anaharibu nyumani kwa majirani lakini anapata backup ya ahera...hafanywi chochote hakamatwi ni kujificha kidogo na kuibuka tena....na huyu kuna walakini kuna watu wanaompa backup ya kuendeleza ukichaa huo....
 
Back
Top Bottom