tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime amesema Jeshi hilo linamtafuta mwanamke aliyeonekana katika picha mjongeo inayosambaa mitandaoni akimnywesha pombe mtoto mdogo na kumtaka atakapoona taarifa hii ajisalimishe mara moja katika kituo chochote cha Polisi.
Misime amesema tukio hilo ni ukatili wa mtoto na ni kinyume cha sheria, zikiwemo Sheria ya Mtoto Sura ya 13 ya mwaka 2023, kifungu cha 9 (3) na 13, pamoja na Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya mwaka 2023, kifungu cha 169 A.
Ufuatiliaji wa kina juu ya tukio hilo umeanza na Jeshi la Polisi limewaomba wananchi wenye taarifa za utambulisho au alipo mwanamke huyo kutoa ushirikiano kwa njia yoyote au kupiga simu kupitia namba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi 0699 998 899.