Aliyemshauri Mbowe agombee alidhamiria kumdhalilisha na kukiua Chama

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Kabisa!

Mbowe itampasa amkumbuke aliyemshauri aendelee kugombea.
Familia yake ilimshauri apumzike, kwa mujibu wa maelezo yake. Ni kwa sababu inampenda na kutaka heshima yake idumu.

Lakini kuna kundi jingine ambalo likamshauri vibaya agombee ili adhalilishwe, heshima yake kushuka, na chama kumfia Mikononi.

Embu fikiria Miaka zaidi ya 30 Mbowe amepigana kufa na kupona kujenga jina na heshima ya brand yake.

Leo hii Mbowe ni wakuitwa Nkurunzinza,
Leo hii Mbowe ni wakuitwa Ayatollah, kweli?

Haya Leo hii Yule Mbowe mwenye jina Kubwa anakuwa kama underground, au underdog kumkabili Lisu mtu aliyemlea Mwenyewe kisiasa? KWELI!

Leo hii Mbowe ni wakushindwa ushawishi kwenye jamii kwa zaidi ya asilimia 80% kila polls zikiitishwa. KWELI?

Heshima iliyojengwa kwa miaka nenda Rudi Leo inavurugika na kupotea kwa Siku chache tuu. Kisa uchaguzi?

Leo hii Mbowe ni wakukataliwa na Robo tatu ya Jamii Forum ambao ni mtandao wa ndani katika nchi yetu. Mtandao unaojitambulisha kama home of Great thinker. KWELI?

Nini kina thamani zaidi ya Heshima? Kitu gani hicho.
Kama ni pesa tayari Mbowe anazo. Nani alimshauri aiweke rehani Heshima yake.

Nani huyo aliyemshauri Mbowe ashindane na Wakati?
Tangu lini mtu akashindana na wakati akashinda zaidi ya kudhalilika na heshima yake kudondoka?

Mfalme Sauli naye heshima yake ilianguka, kwa kushindwa kutambua matumizi ya wakati.
Akawa anapambana na Daudi, kijana mdogo.
Heshima yake yote ikadondoka. Hata Yale mazuri yote aliyoyafanya Sauli Akiwa mfalme yakafutika.

Nawatakia siku njema
 
Kumbe Mbowe alikuwa mvurugaji toka kitambo sana. Ni vile tu hatukujua
 
Mbowe ni jabali la siasa za upinzani Tanzania. Chini ya Mbowe tayari CHADEMA ilishajiunga na FRELIMO, ANC, na Chama cha kikomunisti cha China kama marafiki wa CCM. Lissu ni adui wa demokrasia na kirusi ndani ya chama rafiki CHADEMA.
 
Kwani amekiuka kipengele gani kwenye katiba?

Mkuu Mbowe hajavunja Sheria za kikatiba.
Ila kavunja Sheria za wakati ndio maana unaona yanayoendelea.

Watu wenye AKILI kubwa wanajua kuna Sheria za Wakati.

Waingereza Kipindi cha ukoloni walijua matumizi sahihi ya wakati. Ndio maana muda ulipokwenda Sana wao waliamua kuyapa makoloni Yao Uhuru. Na mpango wao ulifanikiwa mpaka hivi Leo.
 
Mbowe ni jabali la siasa za upinzani Tanzania. Chini ya Mbowe tayari CHADEMA ilishajiunga na FRELIMO, ANC, na Chama cha kikomunisti cha China kama marafiki wa CCM. Lissu ni adui wa demokrasia na kirusi ndani ya chama rafiki CHADEMA.

Mbowe mlichomfanyia sio halali.
Kumshusha Mpaka chini aiseeh

Hakuna Jambo Baya kama character assassination.
 
Bado ananafasi ya kubadili mawazo, vinginevyo hatokuwa na tofauti na lipumba
 
Labda anataka aonyeshe maana ya demokrasia kwa vitendo kwamba akishindwa anatoka.
 
Bado ananafasi ya kubadili mawazo, vinginevyo hatokuwa na tofauti na lipumba

Watu wanaroho mbaya Sana.
KWELI nguvu za jamaa zinaenda kwenda bure Kabisa.

Jina linaanguka chini.
Heshima yote chini hata wale waliomshauri watamkimbia.
Chama nacho kitamfia.

Aliyemshauri amemfanyia ubaya ubwela
 
Back
Top Bottom