Moja ya sifa kubwa na bora ya kiongozi ni kutambua majira na nyakati za kufanya maamuzi sahihi...
Bwana Freeman Mbowe ktk uchaguzi huu ndani ya CHADEMA ameonesha kuwa, huyu kumbe hakuwa kiongozi bali mpigania tumbo lake tu...
Kiongozi gani unayeshindwa kuandaa kiongozi wa kurithi kijiti cha uongozi wako? Anawezaje kupambana na Makamu Mwenyekiti wake wakati ndiyo ilikuwa fursa yake ya kujivunia kuwa ameandaa mrithi bora na akahakikisha anakalia kiti hicho...?
Ndugu
Robert Heriel Mtibeli hakuna haja ya kulaumu washauri hapa...
Wa kujilaumu ni yeye meenyewe Freeman Mbowe kwa kushindwa kutumia vyema akili zake mwenyewe kufanya maamuzi sahihi...
Ameshindwa kabisa kuelewa kwamba, chaguzi za 2009, 2014 na 2019 chama na wanachama walisimama pamoja naye kumpigania aendelee kukiongoza chama hata alipopigwa vita na kuitwa kila jina baya na wapinzani wake CCM kwa kuwa hakuwepo mtu sahihI, makini na mwaminifu asiyehongeka au asiyeweza kukiuza na kukitelekeza chama kurithi mikoba yake...
Lakini safari hii, yupo mtu sahihi kabisa na mwenye sifa zote muhimu na za ziada kurithi mikoba yake kuongoza chama hiki muhimu ambaye ni Tundu Lissu na kila mtu wakiwemo CCM wenyewe wanajua kabisa, huyo jamaa hawezekaniki, hahongeki na yuko straightforward, mkweli, jasiri, na sifa zinginezo njema zote...
Kwanini yeye na chawa wake hawaoni hili?
Mimi nafikiri acha karma iamue.
Mission ya CCM na serikali yake tangu miaka hiyo ni kuifuta au kuiua CHADEMA systematically. Naona mission inakwenda kuwa accomplished chini ya Mbowe huyuhuyu...!!