Uchaguzi 2020 Aliyemshauri Rais Magufuli alipatia, Kama asingezuia shughuli za kisiasa kwa muda wa miaka 5, uchaguzi huu angeshindwa vibaya sana

Uchaguzi 2020 Aliyemshauri Rais Magufuli alipatia, Kama asingezuia shughuli za kisiasa kwa muda wa miaka 5, uchaguzi huu angeshindwa vibaya sana

Achana na Story za kwenye vijiwe vya kahawa wewe, upinzani wana mabadiko gani

Wanaona ajira ndio pointi, ajira ni tatizo dunia nzima, hao wapinzani wasikudanganye kwamba wakiingia ikulu wataajiri kila mtu anayehitimu labda kama wanataka waiingize nchi kwenye madeni yasiyolipika yatayopelekea wadai kuchukua miundombinu ili wajilipe kama ilivyo kwa ndugu zetu hapo...
Acha utahila tanzania tumekosa uongozi wenye kujitambua kama tukipata viongozi wenye nia njema na taifa letu sio tu tunaweza kuajiri watanzania wote bali pia majirani zetu.
 
Kama una limit ya kufikiri usipende kusema umeelewa hadharani. Ulichonasa wewe sicho nilichotega. Si ajabu unakesha sana jitahidi kulala uboreshe ubongo wako. Kama una uthibitisho kuwa hakujawa na ajira kwa takribani miaka 5 ulete. We kama umekosa ajira endelea kuomba Mungu akusogezee siku yako lakini usisingizie hajaajiri watu wanakula vitengo kila leo.
Poor you!
 
Achana na Story za kwenye vijiwe vya kahawa wewe, upinzani wana mabadiko gani kama sio upuuzi mtupu.

Wanaona ajira ndio pointi, ajira ni tatizo dunia nzima, hao wapinzani wasikudanganye kwamba wakiingia ikulu wataajiri kila mtu anayehitimu labda kama wanataka waiingize nchi kwenye madeni yasiyolipika yatayopelekea wadai kuchukua miundombinu ili wajilipe kama ilivyo kwa ndugu zetu hapo, mapato ya airport na shirika lao la umeme yanaenda nje moja kwa moja kwa sababu ya madeni makubwa, kama hicho ndo tunataka tumpe nchi yule anaetumia ajali kuombea kura, eti maumivu aliyopata hatakubali mtu mwingine ayapitie, nani kasema wananchi tutapigwa risasi? Kifupi upinzani hamna jipya.
Unajua ni nini huwa kinasababisha uwepo wa ajira. Sera za Rais Magufuli zimeua vyanzo vya ajira.

Unaposababisha ndani ya miaka 5, kwenye sekta moja tu, makampuni zaidi ya 150 kufunga na kuondoka nchini mwako, unajua ni ajira kiasi gani umeua? Unajua ni kwa kiasi gani unakuwa umesababisha kusinyaa kwa mzunguko wa fedha?

Ujenzi/ukuuaji wa uchumi unahitaji sana akili na mipango kuliko nguvu. Katika awamu hii ukuaji wa sekta zote za uchumi umeshuka. Hiyo ina maana na ukuaji wa ajira katika sekta hizo hizo utakuwa umeshuka lakini pia husababisha kushuka kwa ajira katika sekta za huduma.

Hakuna sekta ya uchumi hata moja ambayo imeongezeka ukuuaji wake katika awamu hii. Zote zimeshuka. Ukuuaji wa sekta ya utalii umeshuka, sekta ya madini umeshuka, sekta ya kilimo umeshuka, uwekezaji kwenye sekta zote umeshuka - hali ikiwa hivyo, ukuuaji wa ajira utatoka wapi, ukizingatia idadi ya watu na watafuta ajira daima inakua.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kuna wasomi kwa akili zao wanasoma ili waje waajiriwe?

Kabisa kabisa wana akili timamu?

Hebu jiulize vyuo vingapi kwa mwaka vitatema wahitimu na kiasi gani?

Halafu dunia inaendelea na teknolojia za kurahisha kazi. Na wasomi wanasoma hayo.

Wasome kujiajiri, sio kuajiriwa, waombe mazingira yawe rahisi kujiajiri. Kuwa na simu tu, kumeondoa ajiri nyingi shirika la posta, machapisho ya stamp, bahasha. Nani anakimbilia kumiliki sanduku hapo posta.

Simu na kompyuta tu imeondoa ma sekretari, wasambaza barua masijala email inatosha. Hoja hizi awe ccm, cdm udp au yeyote hawezi kuniambia nitamuona tapeli.

Hata kuwa watu wanakuahidi vitu kana kwamba wewe ni mtoto, wengine turuhusiwe kuwauliza papo kwa papo wakijichanganya TUWAPIGE ON THE SPOT

Ni hayo tu
 
Najaribu kuwaza Kama tokea 2015 Rais Magufuli angeruhusu shughuli za kisiasa kuendelea Kama ilivyokuwa kipindi Cha nyuma, na hivyo Wapinzani kupata fursa ya kufanya mikutano ya kisiasa Mara kwa Mara ili kuwaambia wananchi juu ya madudu ambayo yamefanyika ndani ya miaka 5, Basi uchaguzi wa mwaka huu Magufuli angeshindwa vibaya sana.

Alicheza karata zake vizuri, ingawa pamoja na Kwamba wapinzani wote walizibwa midomo, wakafungwa kamba wasifanye siasa, na hivyo yeye pekee kuzunguka nchi nzima kuwaeleza wananchi Yale anayoyafanya, lakini bado inaonyesha watu wanataka mabadiliko. Upinzani unaonekana kupokelewa kuliko kawaida. Pamoja na kwamba watu wamepigwa swaga za madaraja, barabara, Ndege n.k lakini wanataka maisha Bora, ajira na huduma nzuri za afya, vitu ambavyo wamevikosa katika awamu hii.
Magufuli phd ni rais wanyonge
 
Mleta mada, kilichowatisha ni ichaguzi wa mwaka 2015.

Wanajua vizuri kabisa kuwa mwaka huo hawakutuboa!.

Mamvi aliogopa tu kukomaa na kudai chake!
 
Achana na Story za kwenye vijiwe vya kahawa wewe, upinzani wana mabadiko gani.

Wanaona ajira ndio pointi, ajira ni tatizo dunia nzima, hao wapinzani wasikudanganye kwamba wakiingia ikulu wataajiri kila mtu anayehitimu labda kama wanataka waiingize nchi kwenye madeni yasiyolipika yatayopelekea wadai kuchukua miundombinu ili wajilipe kama ilivyo kwa ndugu zetu hapo...
Yani ww ushindwe kutimiza wajibu wako km baba watoto walale na njaa afu useme mbona hata jirani yako amelala na njaa? Its a dog shit!! Usihalalishe matatizo yako kwa kuwa na wengine wanayo.. be unique and show the way to escape from sobibo camp!
 
Huo mkakati wa Magufuli kuwanyanyasa wapinzani kwa miaka hii mitano ndio itakuwa kaburi lake kwani yeye ametamba peke yake muda wote huo na hivyo kuwakinai watu.

Sasa wananchi wanataka kuwasikia wale ambao hawakupata fursa ya kuwasikiliza hapo awali na hapo ndipo Lissu anakuwa kama "The Roving Midfielder" huku Magufuli akiwa "Substituted".
 
Yani ww ushindwe kutimiza wajibu wako km baba watoto walale na njaa afu useme mbona hata jirani yako amelala na njaa? Its a dog shit!! Usihalalishe matatizo yako kwa kuwa na wengine wanayo.. be unique and show the way to escape from sobibo camp!
Umempa jibu zuri Sana huyo mjinga
 
Asante kwa kufungua kwamba mwaka huu Magufuli atashinda
Haujanielewa. Kuna kushindwa kawaida na kushindwa Sana. Mwaka huu atashindwa lakini siyo kwa kwa kiwango ambacho angeshindwa Kama asingezuia shughuli za kisiasa
 
Hivi kuna wasomi kwa akili zao wanasoma ili waje waajiriwe?

Kabisa kabisa wana akili timamu?

Hebu jiulize vyuo vingapi kwa mwaka vitatema wahitimu na kiasi gani?

Halafu dunia inaendelea na teknolojia za kurahisha kazi. Na wasomi wanasoma hayo.

Wasome kujiajiri, sio kuajiriwa, waombe mazingira yawe rahisi kujiajiri. Kuwa na simu tu, kumeondoa ajiri nyingi shirika la posta, machapisho ya stamp, bahasha. Nani anakimbilia kumiliki sanduku hapo posta.

Simu na kompyuta tu imeondoa ma sekretari, wasambaza barua masijala email inatosha. Hoja hizi awe ccm, cdm udp au yeyote hawezi kuniambia nitamuona tapeli.

Hata kuwa watu wanakuahidi vitu kana kwamba wewe ni mtoto, wengine turuhusiwe kuwauliza papo kwa papo wakijichanganya TUWAPIGE ON THE SPOT

Ni hayo tu
Kwa hiyo wewe Kama hautaki wasomi waajiriwe unataka kila msomi akimaliza ajiajiri, Kama ikiwa hivo piga picha baada ya miaka kumi kila mtu atakuwa mtaani kuuza nyanya, au kufanya ujasiriamali, Je hapo ndo nchi itakapoendelea? Mfano mtaa mzima wote mnauza nyanya au wote Ni wajasiriamali.
 
Back
Top Bottom