Samia anakuja kuongeza hasira za vijana kuandamana badala ya kuja kuponya majeraha.
Najua atasema, vijana walilipwa, akijua anawatetea kumbe ni dharau kwao kuwa hawana akili ya kuamua mustakabali wa maisha yao hadi walipwe.
Atasema, walioandamana hawakuwa watanzania, wakati waliokamatwa, walio mahabusu na wanaozika wote ni vijana watanzania.
Najua atasema vijana walifuata mkumbo na kudanganywa na wanaharakati wa nje waliolipwa kuichoma nchi yao na ataongezea nasikia kuna kijana kalipwa hadi bilioni 5.
Najua atazungumzia uharibifu wa vitu badala ya uhai wa vijana waliopoteza maisha yao.
Najua atasema serikali imetenga fungu kukarabati miundombinu iliyoharibiwa badala ya kuzungumzia fidia kwa familia zilizopoteza ndugu zao.
Najua atalipongeza jeshi la polisi na vikosi vya ulinzi na usalama badala ya kusema polisi, yeyote aliyehusika na mauaji atawajibika.
Najua atataja orodha na idadi ya vitu vilivyoharibiwa badala ya kutaja idadi ya vifo vilivyotokea.
Najua atasema nchi haiingiliwi wala kupangiwa na nchi yeyote na atasema tuiachie tume yetu ije na mapendekezo yake.
Najua ataongelea nchi wahisani kusitisha misaada, atasema hatutokufa njaa na miradi yote itajengwa kwa pesa zetu wenyewe.
Najua atasema nchi jirani zinatuonea wivu, zinatamani rasilimali zetu zinataka kutuvuruga tuwe kama wao.
Hayo yote hayatasaidia kuponya majeraha kama serikali haitakiri makosa na pengine yataongeza joto la maandamano yaliyopangwa kufanyika Desemba 9.
=!==!!=!=!!==
Ameshauriwa afanye yafuatayo.

- ahutubie kutoka kichwani.
- awatazame watu machoni
- aombe radhi kwa yaliyotokea.
- aombe mazungumzo na waathirika!.
- aahidi mabadiliko makubwa
- akemee utekaji.
- aombe kuzungumza na Gen Z.