Aliyemteketeza mkewe kwa magunia mawili ya mkaa ahukumiwa Kunyongwa mpaka Kufa

Aliyemteketeza mkewe kwa magunia mawili ya mkaa ahukumiwa Kunyongwa mpaka Kufa

#HABARI: Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo Februari 26,2025 imeanza kusoma hukumu ya kesi ya mauaji, inayomkabili Mfanyabiashara Khamis Luwonga (38), anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa.

Katika kesi hiyo ya mauaji namba nne ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

#Follow @radioonetanzania
Mbona Jamaa alishawaambia muda Sana wamhukumu?! Why wamechelewesha?
 
#HABARI: Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo Februari 26,2025 imeanza kusoma hukumu ya kesi ya mauaji, inayomkabili Mfanyabiashara Khamis Luwonga (38), anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa.

Katika kesi hiyo ya mauaji namba nne ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

#Follow @radioonetanzania

Hachomoki 😭😭
 
Jamaa alikuwa bado hajakomaa kima penzi... Mimi naulinda wangu moyo. Simuamini hata mkewangu najua muda wowote ananisaliti huko njee. Maana na mimi huwa namsaliti maana shetani yupo hai..

Nime seti hivyo akili yangu bila kujali ni kweli au si kweli. Ni uchizi kiwango cha PhD kuamini mke wako ni wako peke yako. Hasa kiwa na wewe hutoka na wake za watu. hivyo sina muda wa kumfuatilia. Na ukitaka mwanamke akudharau basi aijue akili yako juu yake..

Itoshe kuamini kumpuuzia mkeo ndiyo maana yake siyo ujinga bali ni ukomavu.. Wa Hisia... Zako.
 
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo Februari 26,2025 imeanza kusoma hukumu ya kesi ya mauaji, inayomkabili Mfanyabiashara Khamis Luwonga (38), anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa.

Katika kesi hiyo ya mauaji namba nne ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

=======

Kijana Khamis Luwonga (45) maarufu Meshack aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kumuua mke wake, Naomi Marijani na kisha kuuchoma mwili wake kwa kutumia magunia mawili ya mkaa amehukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Hukumu hiyo imetolewa leo Februari 26,2025 na Jaji Hamidu Mwanga wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi 14 wa upande wa Jamhuri ambao wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mtuhumiwa ametenda kosa hilo.

Luwonga alimuua mkewe Naomi na kisha kuuchoma moto mwili wake kwa kutumia magunia mawili ya mkaa nyumbani kwao eneo la Gezaulole, wilayani Kigamboni, Dar es Salaam Mei 15, 2019.

Baada ya kuuchoma mwili huo ndani ya banda la kuku, alienda kuzika masalia ya mwili huo na majivu shambani kwake na kupanda migomba juu yake.

TBC
Ndoa za siku hizi zina changamoto kubwa sana kupita kiasi.
Hapo ndipo wale Watu wa Kampeni ya Kataa Ndoa wanapokuwa na Hoja zenye mashiko na ndipo wanapopata Wafuasi wengi sana wa kuwaunga mkono.
 
Back
Top Bottom