Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Kuna vitu vingi sana nimejifunza kwenye hii kesi ya mauaji na huenda ikawa na faida kwa wengi;Tate Mkuu babu soma kisa hiki.
1. Ni kosa kubwa kwa mwanaume kukubali sharti la mwanamke la kubadili dini ili muoane. Hapa lazima utanyanyasika tu siku za usoni. Maana umemuonesha kuwa unampenda sana, jambo ambalo mwanamke hatakiwi kuoneshwa! Kwa sababu mara nyingi hulitumia kama silaha ya kukunyanyasa.
2. Ni kosa kubwa sana kuoana na mtu ambaye mna tofauti nyingi kati yenu. Yaani hamuendani kuanzia muonekano, umri, elimu, mtazamo, mahusiano, tabia, maisha, fikra, nk.
3. Maisha ya ndoa yanahitaji uvumilivu. Ila usipitilize. Na hapa ndipo wenzetu Wazungu wanapotuzidi. Wenyewe wakiona mambo yamekuwa ni magumu, wanaachana. Ila sisi tunalazimisha, na mwisho wa siku matokeo yake ndiyo haya.
All in all, namsikitikia sana huyu jamaa. Kwa muonekano wake tu utamgundua amepitia matatizo mengi sana ya kisaikolojia kutokana tu na ndoa yao kukosa uaminifu, furaha, amani, upendo na mshikamano.
Na inahuzunisha zaidi maisha yao wote wawili yameharibika kwa sababu tu ya ubinafsi wao! Inahuzunisha zaidi na zaidi kwa mtoto Gracious ambaye amempoteza mama yake, huku na baba yake naye akiishia jela. Kwa kweli inaumiza na kuhuzunisha san mjukuu wangu! ☹️