Aliyemuua askari Arusha adaiwa kufa akijaribu kuwatoroka polisi

NJIA PEKEE YA KUMALIZA TATIZO LA UJAMBAZI, NI HILI LA JAMBAZI KUJARIBU KUTOROKA AKIWA CHINI YA POLISI. SAFI SANA
 
Polisi mtajibu kwa Mungu.... hata kama ni jambazi, kuna utaratibu
 
I smell rat!Hizi story za kawaida,huyu amekuwa executed,porini harafu vitu vikawa stage managed,polisi ccm ndio zao,hawana akili
 
Umekuja na uCHADEMA speed 160,rudi kasome upya alichoandika mtoa mada.
 
Umekuja na uCHADEMA speed 160,rudi kasome upya alichoandika mtoa mada.
Nimesoma alichoandika na nimesoma uzi wa huyo askari kuuwawa na mazingira yaliyoelezewa. Hiyo comment yangu haijaanzia kwenye uzi huu, sijakurupuka.
 
Haaaa huyu atakuwa wamemdedisha tu! Wajua kwa sasa ishu za majambazi hakuna ku negotiate nao ni kuwa murder tu kupunguza kazi.
 
Polisi polisi polisi. Unawezaje kuruka kwenye gari ukiwa umefungwa pingu mikononi? Iundwe kamati ya kuchunguzwa kifo hicho.
Inqmaqnq toka Moro hadi Arusha ni kwa gari gani pick-up au suv haina child lock?!
Hapo ndipp utaelewa jamaa hawakutaka mlolongo wa mambo na huyo jambazi kichwa.
 
Maana yake ni kuwa ukizingua na wewe unazinguliwa. Kuua watu na kuharibu maisha ya wengine, mwisho wake ni kuuwawa
Huenda askari aliuawa kwenye fumanizi au hata akiwa kwenye harakati za yeye kufanya Ujambazi. Na huyo anayeitwa mtuhumiwa wala siyo mhusika kiuhalisia Ila amebambikwa, akapigwa, akafa kisha tunakuja kuambiwa amejirusha ili mambo yaishe na kusiwepo na mwendelezo utakaofichua ukweli wa kilichomuua Askari mwenzao.

Polisi wetu sina imani nao hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…