Aliyemteketeza mkewe kwa magunia mawili ya mkaa ahukumiwa Kunyongwa mpaka Kufa

Aliyemteketeza mkewe kwa magunia mawili ya mkaa ahukumiwa Kunyongwa mpaka Kufa

Pascal_TZA

Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
27
Reaction score
76
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo February 26,2025 imemhukumu kunyongwa hadi kufa Mfanyabiashara Khamis Luwonga (38) kwa kumuua Mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa

Katika kesi ya jinai namba 44/2023 mfanyabiashara huyo mkazi wa Gezaulole, wilayani Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa kumuua mkewe Naomi Marijani kinyume cha kifungu cha 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, kama ilivyorejewa mwaka 2019.

Pia soma Mahakamani: Aliyemchoma mkewe kwa magunia mawili ya mkaa anatajwa kuwa mlemavu wa akili

Anadaiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2019 nyumbani kwao kisha akauchoma mwili kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ndani ya banda la kuku. Inadaiwa masalia ya mwili na majivu alikwenda kuyazika shambani na kupanda migomba juu yake.

View: https://youtu.be/ydRPqeEjo68?si=Qn2ebxb1IO-8N9-z

IMG_1186.jpeg
 
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo Februari 26,2025 imeanza kusoma hukumu ya kesi ya mauaji, inayomkabili Mfanyabiashara Khamis Luwonga (38), anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa.

Katika kesi hiyo ya mauaji namba nne ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

=======

Kijana Khamis Luwonga (45) maarufu Meshack aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kumuua mke wake, Naomi Marijani na kisha kuuchoma mwili wake kwa kutumia magunia mawili ya mkaa amehukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Hukumu hiyo imetolewa leo Februari 26,2025 na Jaji Hamidu Mwanga wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi 14 wa upande wa Jamhuri ambao wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mtuhumiwa ametenda kosa hilo.

Luwonga alimuua mkewe Naomi na kisha kuuchoma moto mwili wake kwa kutumia magunia mawili ya mkaa nyumbani kwao eneo la Gezaulole, wilayani Kigamboni, Dar es Salaam Mei 15, 2019.

Baada ya kuuchoma mwili huo ndani ya banda la kuku, alienda kuzika masalia ya mwili huo na majivu shambani kwake na kupanda migomba juu yake.

TBC
1740576622521.jpeg
 
Back
Top Bottom