Aliyeng'atwa na Nyoka afia Kituo cha Afya kisa hana 150,000 Wilayani Babati

ni u jinga wa hali ya juu kuisingizia ccm kwa hili hao wauguzi unajuwaje kama ni ccm au chadema? wachukuliwe hatua kali sana siyo kukaa na kuilaumu ccm mingine michadema iliyoishiwa hoja inauwa watu makusudi ili isingiziwe ccm
 
Eeh Mungu wangu hiki ni nini jamani mbn inasikitisha mno mtu kashasema kangatwa na nyoka badala ya kuangaza kuhangaika kumsaidia mambo mengine yafuate inaangaliwa kwanza hela ndio ahudumiwe mwisho wa siku kafa.Nyinyi madaktari huko chuo mmefundishwa kuzoea kifo au kuokoa watu wanaokufa.Sasa amekufa andaeni cheti cha kifo sababu hicho ndicho mlichokuws mnakitaka.HII NI AIBU KWA MADAKTARI NA WAUGUZI
 
Watumishi wa afya hawana makosa .

Ya kulaumiwa ni serikali, mifumo yao ya uendeshaji ni mibovu na lawama huwa wanawaachia watumishi .
Sio kweli ,uyo mpaka anafika pale sio mkazi wa mbali na eneo husika , yani katika emergency ya mgojwa unatanguliza pesa kwanza ayo ndo maelekezo ya serikali katika vituo vya kutolea huduma? Mfano mtu amepata jeraha anableed na unaona is life threatening so unaanza pambana na pesa au kumuweka sawa mgonjwa then pesa ?

Mengine watumishi wabovu wanaifanya Serikali kubeba lawama bila sababu, mfano kuna vituo vya afya wakati serikali inasema mama mjazito ,watoto chini ya miaka 5 ni bure , wao huwatoza pesa kisa eti wanakusanya mapato ,je hapa serikali inalaumiwa kwa lipi ili hali mwongozo upo wazi?

DMO wapo ,wakurugenzi wapo, madiwani wapo,wabunge wapo, wakuu wa wilaya wapo.
 
Hao wauguzi na madaktari uwakute Jumapili au Ijumaa kwenye makanisa na misikiti yao wakisali wapo mbele kabisa.Njoo huku uone wanachofanya mtu anakata roho wanaangalia hivi na hamna anayeshtuka.Hamkupaswa kupewa hizo nafasi sababu daktari au muuguzi ni mtu wa kuokoa maisha ya watu Ila Tanzania ni kinyume chake!
 
Mkuu madaktari wengi wanajitambua , ni hivi vidactari vya sasa vinavyoingia kwenye ajira mpya ndo vinaaribu ,vinaamini kauli yao katika kusimamia vituo ndo kauli ya mwisho
 
Na wahusika hawatachukuliwa hatua yeyote licha ya kusababisha kifo cha mtu.
 
Ha
Hiyo ni kazi kama kazi zingine .Mnahimizwa sana muwe na bima ya afya ila hamzingatii.

Wewe hapo unapofanya kazi unaweza kumuhudumia mtu bure?
Hakuna mwongozo wowote wa serikali unaosema kwamba mgonjwa wa emergency ukimbizane na pesa katika vituo vya umma, ndo maana hata leo akiokotwa mtu amepata ajali na hana ndugu, atatibiwa Mengine yatajulikana badae
 
Mno especially government hospital watu wanateseka sana,mi niliwahi kugombana na mhudumu mmoja tena sikutaka kuyakuza,pamoja na hayo kuna wahudumu wanaipenda kazi yao.
Hawa form four failure wengi ni tatizo
Hakuna cha form four hapa, huduma ya afya imetoka mbali, unajua mwanzo wahudum wa afya wengi walikua la 7, unajua AMO ndo walikua maincharge kwenye hospital za mikoa na wilaya, unajua Co ndo walikua incharge kwenye vituo vya afya kabla , na je huduma zilikua zinaenda au haziendi .

Kishimba ni Mbunge na ni la saba ila anaakili kuliko maprof unajua hilo.

Msukuma ni mbunge na la saba ila yupo na akili kuliko wenye PhD zao apo Bungeni
 
Kuna watu wanaitwa maboss huko maofisini, Hawa ndio chanzo Cha uharibifu, vikao vyao na watumishi ni vitisho, kuvishana hofu na kutetemeshana, hili linasababisha watumishi wa chini kutokutumia akili na utu sababu mda mwingi Wana hofu
Kutojielewa sheria na kanuni za utumishi wa umma zipo pale ,sasa unatetemeka nini, Daktari we si umeapa kutoa huduma kwa wagonjwa bila upendeleo ,sasa hofu ya nini ili hali ulichofanya ni ethical tokana na taaluma yako ,hofu ya nini kama sio uzwazwa
 
As for me,still naona hii theory kwenye suala la afya ya mtu haiingii akilini na wa kulaumiwa bado ni hao waliokuwa eneo la tukio hata ukisoma maelezo ya mganga mkuu anasema mtu akiumwa na nyoka mkali anatakiwa atibiwe haraka so yeye hakuwepo hata kama ndiye alitoa amri matibabu yasifanyike mpaka pesa ilipwe inabidi waliokuwepo watoe huduma sababu wao ndiyo walikuwa wanaona mabadiliko ya mgonjwa hatua kwa hatua.

Labda ingekuwa ni private hospital lakini kwenye hospital za serikali huwa kunakuwa na msamaha wa matibabu pale mgonjwa ameshindwa kulipa bill yake kwanini huyu asingetibiwa maisha yake yaokolewe then pikipiki izuiwe ikija kutokea utata baadae aingizwe kwenye program ya msamaha?tunarudi pale pale kwamba hao waliokuwepo hawana wito wa udaktari yaani kabisa mnamuona mtu anakaribia kukata roho mbele yenu nyie bado mnakaza lete hela lete hela?

Watu huruma hawana kabisa yani mke wa mtu mzazi wa mtu anayetegemewa anakata roho mbele yenu nyie mnamtizama tu?wakati dawa zipo na siyo zenu?na mmepewa bond ya pikipiki ya approximately 800K hata angetokea mmoja akawa dhamana akachukua yeye pikipiki huyo mama akatibiwa,umaskini m'baya sana na unakuwa m'baya zaidi ukikutana na watu wenye ufinyu wa kufikiria na roho mbaya.
 
Kutojielewa sheria na kanuni za utumishi wa umma zipo pale ,sasa unatetemeka nini, Daktari we si umeapa kutoa huduma kwa wagonjwa bila upendeleo ,sasa hofu ya nini ili hali ulichofanya ni ethical tokana na taaluma yako ,hofu ya nini kama sio uzwazwa
Hujui wa Tz wengi ni mazwazwa!?,,,

Hizo ethics unazizungumzia zipo Kila mahali , lakini utekelezaji wake ukoje!?

Mara ngapi umesikia simu Toka juu zimebatilisha hukumu mahakamani,Sheria barabarani, vibari vya umiliki wa rasilimali nk ,na ethics zipo wazi!?
 
Huwa pia inategemea ni aina gani ya Nyoka amekugonga maana sio Nyoka wote wana sumu, na hata wale wenye sumu huweza kugonga bila kuachia sumu(dry bite).Ila kwa huduma ya kwanza iliyotolewa inaonesha huyo ni mjuzi maana kuwahi jeraha na kufanya damu itoke inaweza kupunguza kiwango cha sumu..ila kama nilivyosema inategemea na aina ya Nyoka..ila alitakiwa amalize kwa kuwashauri pia muende Hospitali.
 
Mimi nimeelezea ushuhuda wangu kung'atwa na nyoka. Japo wengine wananibishia.

Kutibiwa kwa kutafuna mizizi ya mti nilio pewa na mtaalamu na kukamuliwa juice ya majani Fulani na kubandikwa majani kwenye jeraha la nyoka.

Na mpaka Leo na dunda.
 
Hahaha naufahamu mzima ila sikujua kuhusu hili...

Kuhusu dawa za nyoka ni kweli zipo, maeneo yale mtu akiumwa nyoka haendi hospitali.
Baba yangu mkubwa alipenda kuniambia kua HII MITI INAONGEA.

YAANI AKIWA NA MAANA MITI HUWAGA INAONGEA.

Huko usukumani Kuna mpaka wakamata nyoka na kucheza nao nyoka wanapumbazwa..

Baadae ntatoa kisa Cha bro mmoja alichanjia dawa yaan hata nyoka akimuuma hapati madhara kwa macho yangu NILISHUHUDIA kwenye parking tukifanya usafi akang'atwa na nyoka mkubwa mweusi
 
Mkuu kuweni making na hizi dhana zisizo na ushahidi wa kisayansi.Kuna Watu wanafanya triki tu za kucheza na Nyoka wenye sumu hafifu isiyo hatari kwa biinaadamu au wasio na sumu kabisa mfano Chatu n.k.Tusiwe wepesi wa kuamini jambo Watu wachache tu na kuishia hapo,uwezo wa kuhimili sumu si lingekuwa jambo la Dunia yote ama?Hivi ni Wanasayansi gani wasingependa kumjua Mtu anayehimili sumu kali ya Nyoka au sumu yoyote ile?.Huko kwa Wenzetu kuna Watu wanafanya kazi kwenye maabara zenye aina tofauti karibia elfu moja ya Nyoka na wanachukua tahadhari zote iwapo itatoka akali ya kuchongea nao.
 
Sijui kama hiyo dawa ilikuwepo hapoo kwa level ya kituo cha afya ukute hata friji hawanaa labda walitaji pesa kwanza wakanunue ndipo achomwe so kwa mazingira hayo lawama ni za bureee ubaya kama hiyo dawa ilikuwepo hivyo vituo hata petty cash ya dharura huwa hawanaa.
 
Kutojielewa sheria na kanuni za utumishi wa umma zipo pale ,sasa unatetemeka nini, Daktari we si umeapa kutoa huduma kwa wagonjwa bila upendeleo ,sasa hofu ya nini ili hali ulichofanya ni ethical tokana na taaluma yako ,hofu ya nini kama sio uzwazwa
Unadhani dawa kwenye famasi zinatoka kama nyanya??? kesho ndo mtu akikaguliwa anaambiwa ni mwiziii wa dawa.
 
Hivi unajua ni watu wangapi wanaokuja na excuse za kwamba hawana pesa? Ungekuwa ww ndio mtumishi wa level za chini unadhani ungeonea huruma wangapi ? Na ukumbuke hasara yoyote unayoitengeneza ww ndiyo utalipa.

Huyo Mganga Mfawidhi hawezi kuondoka kituoni bila ku-delegate mamlaka, kwa nini yeye mwenyewe hakuchukua jukumu la kumpigia yule alomkaimisha ampe maelekezo ya nini cha kufanya, unaposema nenda tu wakusaidie maana yake nini?

Ni kweli kwenye hospitali za umma kuna utaratibu wa msamaha wa muda mfupi na mrefu, lkn anayetoa hiyo misamaha ni Waganga Wafawidhi wenyewe, hivyo bado tunarudi palepaleee...

Na ukumbuke nimekuambia ktk dawa ambayo huwa iko strict kwenye kutolewa ovyo ovyo ni hizo ANTI-VENOM, na nimekuambia utaratibu uliopo ni PRE-PAID.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…