Aliyenunua mdoli na kuuweka bungeni ashikwe afunguliwe mashtaka ya uhujumu uchumi

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Mdoli huyu hata vitoto vyenye certificate ya electronic ya pale VETA vinaweza kuujenga.
Mdoli eti mpaka uusogelee usubiri dk kadhaa apate hisia ya kunyoosha mkono .

Mdoli waneupaka rangi ya Tanzania, mdoli hautembei, haujui Kiswahili wala lugha yoyote.
Waliohusika kuununua washikwe wafunguliwe mashitaka ya uhujumu uchumi na udanganyifu kwa umma.

Watanzania wamemaliziwa bandle zao kutazama mdoli ambao hauna maajabu.
 
Ccm sijui wanatuonaje.

Hilo dude labda wamenunua Kariakoo
 
Hivi Wakenya hawajaona jamani?
 
Umetoa mashtaka yasiyo na facts, wamenunua wapi mdoli huyo? hao watoto wa veta kwa nn hawakutengeneza
 
Tuliza makalio. Akili yako ni ndogo kuelewa kwa nini jana Eunice akitumia alili mnemba (Artificial Intelligence) alikuwa ndiye mkaribisha wageni bungeni na kutoa ile summary ya malengo ya wizara ya mawasiliano.

Dunia yote inakwenda kiteknolojia kuanzia elimu, utafiti, vita, usafirishaji na hadi huduma kwa wateja.

Kama Tanzania ita zembea au itazubaa kwenye kwenda ana kasi ya dunia basi itaachwa vibaya kwenye mbio za kujenga uchumi mkubwa na ulio bora.

Kama unaona ile robot Eunice ni mdoli basi na wewe ni mdoli pia japo unatembea mwenyewe.
 
Eunice ni Roboti au sio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…