Aliyeolewa akaachika miaka 7 sasa imepita ila hakupewa talaka, Anataka nimuoe. Je, naweza kumuoa?

Aliyeolewa akaachika miaka 7 sasa imepita ila hakupewa talaka, Anataka nimuoe. Je, naweza kumuoa?

Kwan yeye mleta mada umeujua umri wake?

Alaf swala la umri wa huyo mwanamke na watoto wake, vyote alivijua, na bado akaweza kuishi nae miaka mitatu, hadi wazo la kumuoa likamjia, hajakurupuka.

Na ndio maana ushauri anahitaji umelenga eneo jingine kabisa
Sahihi kbs
 
Unataka kuoa kwa kigezo cha ramadhani?

Mna umri gani kwanza??

Kama unaelekea jion ni sawa ila kama bado inachemka shtuka bro
 
Naishi naye huu mwaka wa 3 bila ya ndoa.

Hadithi yake ya nyuma ipo hivi
" Alioelewa akiwa na miaka 17 baada ya kupewa ujauzito na uyo jamaa na wakaishi wote miaka 8 kwenye ndoa na kuzaa watoto wawili.

Sababu ya kuachana uyo jamaa alianza kula madawa ya kulevya ndugu wakampeleka sober akarudi kwa madai ameacha baada ya muda akarudia tena . Uyu mama akarud kwao jamaa akazama kwenye uteja tena .uyu mwanamke akarudi kwao kabisa. Sasa imepita miaka 7 tokea waachane

Mimi
" Anataka nimuoe kwaajili ya hii ramadhan .na nimeishi nae mwaka wa 3 sasa kama mke na mume

Karibuni
Kwanini asi process taratibu za talaka ?!. Haraka ya nini !
 
Naishi naye huu mwaka wa 3 bila ya ndoa.

Hadithi yake ya nyuma ipo hivi
" Alioelewa akiwa na miaka 17 baada ya kupewa ujauzito na uyo jamaa na wakaishi wote miaka 8 kwenye ndoa na kuzaa watoto wawili.

Sababu ya kuachana uyo jamaa alianza kula madawa ya kulevya ndugu wakampeleka sober akarudi kwa madai ameacha baada ya muda akarudia tena . Uyu mama akarud kwao jamaa akazama kwenye uteja tena .uyu mwanamke akarudi kwao kabisa. Sasa imepita miaka 7 tokea waachane

Mimi
" Anataka nimuoe kwaajili ya hii ramadhan .na nimeishi nae mwaka wa 3 sasa kama mke na mume

Karibuni
Kiwanja chenye mgogoro kinachotembea
 
Unamheshimu Ramadhani unazini mbele ya shabani.
 
Unataka uoe mke wa mtu hapo. Fatilia taratibu za kisheria, ili talaka itoke mkuu. Nadhan kwa situation hiyo, ndugu wa mume wake wa kitambo, hawatakuwa na ubishi kutoa talaka.
Uko sahihi mkuu. Akimuoa wakati ndoa ya awali haijafa basi ndoa yao mpya haitakuwa halali Kisheria.

Cha kufanya, mwanamke apeleke Mahakamani ombi la talaka. Lkn ombi la talaka haliwezi kusikilizwa Mahakamani bila mwanamke kuwa na hati ya Usuluhishi ya maswala ya ndoa kutoka kwenye mabaraza ya usuluhishi yaliyopo misikitini (bakwata), makanisani au kwenye kila kata. Haya mabaraza yatajaribu kuwasuluhisha, ikishindikana, itaandaliwa hati ambayo itaambatanishwa na maombi ya talaka yatakayopelekwa Mahakamani.

Hati ya usuluhishi halitakuwa takwa la lazima kama mwanaume atakataa kwenda kwenye hilo Baraza.

Moja ya sababu ambayo Mahakama itaizingatia kabla ya talaka kutolewa ni wanandoa kutengana kwa zaidi ya miaka mitatu. Mtoa mada anasema huyo mwanamke wake katengana na mume wake kwa miaka 7; so sababu ya msingi ipo.

Apeleke kesi Mahakama ya mwanzo au ya wilaya. Mahakama ikiamua kwamba waachanishwe ndiyo jamaa anaweza kufunga ndoa mpya halali ambayo itatambulika kisheria.

Kwa sasa ni hayo tu, namtakia kila la kheri.
 
Back
Top Bottom