Aliyeolewa akaachika miaka 7 sasa imepita ila hakupewa talaka, Anataka nimuoe. Je, naweza kumuoa?

Sahihi kbs
 
Unataka kuoa kwa kigezo cha ramadhani?

Mna umri gani kwanza??

Kama unaelekea jion ni sawa ila kama bado inachemka shtuka bro
 
Waislamu hawanaga ndoa ndoa zipo Kwa kristo hao wanazinigi tu
 
Kwanini asi process taratibu za talaka ?!. Haraka ya nini !
 
Kiwanja chenye mgogoro kinachotembea
 
Unamheshimu Ramadhani unazini mbele ya shabani.
 
Unataka uoe mke wa mtu hapo. Fatilia taratibu za kisheria, ili talaka itoke mkuu. Nadhan kwa situation hiyo, ndugu wa mume wake wa kitambo, hawatakuwa na ubishi kutoa talaka.
Uko sahihi mkuu. Akimuoa wakati ndoa ya awali haijafa basi ndoa yao mpya haitakuwa halali Kisheria.

Cha kufanya, mwanamke apeleke Mahakamani ombi la talaka. Lkn ombi la talaka haliwezi kusikilizwa Mahakamani bila mwanamke kuwa na hati ya Usuluhishi ya maswala ya ndoa kutoka kwenye mabaraza ya usuluhishi yaliyopo misikitini (bakwata), makanisani au kwenye kila kata. Haya mabaraza yatajaribu kuwasuluhisha, ikishindikana, itaandaliwa hati ambayo itaambatanishwa na maombi ya talaka yatakayopelekwa Mahakamani.

Hati ya usuluhishi halitakuwa takwa la lazima kama mwanaume atakataa kwenda kwenye hilo Baraza.

Moja ya sababu ambayo Mahakama itaizingatia kabla ya talaka kutolewa ni wanandoa kutengana kwa zaidi ya miaka mitatu. Mtoa mada anasema huyo mwanamke wake katengana na mume wake kwa miaka 7; so sababu ya msingi ipo.

Apeleke kesi Mahakama ya mwanzo au ya wilaya. Mahakama ikiamua kwamba waachanishwe ndiyo jamaa anaweza kufunga ndoa mpya halali ambayo itatambulika kisheria.

Kwa sasa ni hayo tu, namtakia kila la kheri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…