Pre GE2025 Aliyepinga Rais Samia kupitishwa Mgombea pekee wa Urais kupitia CCM afukuzwa uanachama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa ninavyowajua CCM na dola walivyo na nongwa hapo hawajamalizana naye, lazima watampeleka kaburini tu, tukifanya rejea ya kilichomkuta yule dogo Chaula aliyechoma picha ya Samia, mahakama ilimtia hatiani na akahukumiwa kifungo au faini, wasamaria wema wakamchangia faini akawa huru lakini hawakuridhika wakamteka na kumpoteza hadi leo maiti yake haijaonekana.
 
 
Ana bahati hajatekwa, maana ccm mmh ni balaa
 
ameweka rekodi mpya kwa chama cha mafisadi na taifa,ccm wasisahau kumuingiza kwenye rekodi yao kwamba kuna mwaka walifanya ujinga ila malisa alipinga
 
Hata Saddam Hussein na Gaddafi walitisha sana watu wa hali ya chini, ila kiko wapi mpaka leo hii. Ni suala la muda tu, all these shall come to an end.

....and not just an end, but a shameful ending.
 
Hahahha ccm kweli hawana haya napigania katiba imekiukaa alafu waliokiuka katiba wanamfukuza chamani hiyo ni mwizi anamfukuza mwizi.
Ccm dah hadi huruma
 
Huyo Malisa hakujua kuwa ndani ya chama chetu ccm hakuna demokrasia?!
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, kimemfukuza uanachama kada wa chama hicho Mchungaji Godfrey Malisa kuanzia leo Februari 10, 2025 kwa tuhuma za kukiuka Katiba na maadili ya Chama hicho.

Hatua ya kufukuzwa kwa Malisa imeelezwa kuwa inatokana na kauli alizokuwa akizitoa kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa Januari 19, 2025 akidai kupitisha kwa wagombea hao (Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania Bara) na Dk Hussein Mwinyi- Zanzibar) kumekiuka Katiba ya CCM.

Mchungaji Malisa, ambaye amewahi kugombea urais, uspika na hata ubunge, alijiunga na CCM mwaka 2021 na alikuwa miongoni mwa makada tisa waliochukua fomu kugombea uenyekiti wa Chama hicho mwaka 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 10, 2025 Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Merce Mollel amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya mkoa.


Mwananchi ilipomtafuta Dk Malisa kuhusiana na uamuzi huo, amesema kuwa hakupewa taarifa wala kushirikishwa.

Endapo, mwanachama huyo amefukuzwa kwa sababu za kinidhamu kama inavyodaiwa na hakushirikishwa katika zoezi hilo kama anavyodai, basi CCM - Kilimanjaro itakua imevunja Katiba ya Chama cha Mapinduzi kwa mujibu wa kifungu cha 14(4) kama kilivyowekwa hapo juu.
 
Amefukuzwaje bila yeye kuwa na taarifa?

Barua ya kufukuzwa iko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…