PreGE2025 Aliyepinga Samia na Nchimbi kupitishwa kama wagombea Urais CCM, apeleka shauri lake mahakamani kupinga ukiukwaji wa Katiba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huyu jamaa historia yake amekuwa mtu wa kuhama hama vyama vya siasa ... Aondoke tu CCM... Wana CCM tumeridhika na mama..
 
Katangulizwa tu huyu, ila nyuma yake usushangae kukuta hata kina Lucas Mwashambwa au Tlaatlaah wamo

Huko CCM unafiki na usaliti ni mkubwa mno. Usione wanachekeana mchana, usiku kila mmoja hukimbilia kwa shetani wake wa kumsaidia
Yaani,
mgombea urais wa chama cha cck analalamikia taratibu za ndani za CCM?
huo si ushirikiana ulio ambatana na tatizo la afya ya akili gentleman?🐒
 
yaani CCM ibabaike na mgombea urais wa chama cha cck ambae ana historia ya tatizo la afya ya akili, surely?

kwa huruma na kujali utu wa kila mwanadamu, CCM haitasita kumsaidia na hatimae atakaa sawa na kuendelea vyema na harakati za kisiasa. Ugumu wa maisha ni kitu mbaya sana ndrugu zango 🐒
 
Mungu amsimamie huyu baba. Sote tuko nyuma yake na malaika wa mbinguni wamemzunguka.

Samia amebaka demokrasia ndani ya ccm na nchi kwa ujumla.
 
Mwenyekiti aligoma kutoka nje,acha kutufanya wajinga kama wewe,nenda kacheki upya mkutano mkuu,kama hukuwepo dodoma au ulisinzia au ulienda chooni kuhara.

Ila hoja ilitolewa na kibajaji akagomea wajumbe tena wa mkutano mkuu.

Ccm imegeuka kuwa genge la wahuni
 
Tulia bro..

Hujui nini kinaendelea ndani ya CCM na serikali kwa sasa...

Kuna kambi mbili kwa sasa humo. Zote ni so powerful....

Tunasema hivi, yajayo yanafurahisha bro....!

Kaa mkao wa kuiona Tanganyika ikirudi toka kuleeeeeeeee ilikofichwa...
Mkuu, kwa muda wote huo bado hiyo Tanganyika yako itakuwa haijaoza kweli? Sijui, ngoja tuone IKITOKA.
 
Mzee ana hoja ajibiwe, tulionya sana ,kilichofanyika ccm ni haibu
 
Huyo bila shaka atakuwa kijani mwenye utambuzi akiyeukataa uchawa, kama ule wa mitano mingine.
 
Ha haa
hadithi hii inatufundisha nini!?
 
Mzee ana hoja ajibiwe, tulionya sana ,kilichofanyika ccm ni haibu
no gentleman plz,
ana matatizo ya kibinafsi ya kihistoria, atasadiwa tu kwanza kijamii ili akae sawa, kisheria na kiuchumi angalau apunguze fedheha anazopitia maishani kama mtu mzima 🐒
 
Kiasi fulani kuna watanganyika watakuwa wamepata kamwanga kiasi kuhusu nini
Kinaendelea kwenye nchi yao ambayo

Wachache uchagua nani ake wapi nani awe nani

Such shit
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…