Bonus kwenye sports industry ipo kisheria mfano man utd kila inapovuka hatua champions league kuna kiasi mchezaji anapata (ni % chache ya mshahara), timu isipofanikiwa kuingia uefa champions league wachezaji wanakatwa 25% ya mshahara kwa msimu nzima. Mfumo huu unatumika karibu timu zote kubwa, iwapo timu itashuka daraja mshahara unakatwa karibu nusu na zaidi.
Leicester city wamereport loss ya paund mil 37 msimu uliopita. Hata simba tunatakiwa tusomewe taarifa ya revenues za robo, nusu, robotatu na mwaka tuone tunapoelekea kwasababu tunasema sisi ni next level.
Hakuna kitu kigumu kama kutengeneza profit kwenye sports industry