Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi Mei 19, 2026 imemuachilia huru kwa kumfutia KESI ya UHAINI Mchungaji Godfrey Malisa, kwa masharti kwamba asifanye kosa ndani ya Miezi 12.
Picha hii imeboreshwa na AI
Dkt. Godfrey Malisa alikuwa anakabiliwa na kesi mbili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, ambazo;
Zaidi soma
Picha hii imeboreshwa na AI
- Kesi ya uhaini namba 000028333 ya 2025, ambapo anadaiwa kuhamasisha umma kushiriki katika mikusanyiko isiyo halali kwa kumtishia Rais Samia kujiuzulu la sivyo yangefanyika maandamano makubwa nchini Desemba 9, 2025.
- Kesi ya Makosa ya Kimtandao namba 000028411 ya 2025, ambapo anatuhumiwa kuchapisha taarifa katika kurasa yake ya Youtube Novemba 2025, akimtaka Rais Samia kujiuzulu kwa kuhusika na vifo vya maelfu ya Watanzania, akifahamu kuwa taarifa hizo si sahihi zilizolenga kupotosha umma.
Zaidi soma
- Dkt. Malisa: Rais Samia ajiuzulu kabla ya Disemba 9 au Akabili Maandamano makubwa ambayo hayajawahitokea Barani Afrika
- Aliyekosoa mchakato wa uteuzi wa Samia ndani ya CCM, Mzee Godfrey Malisa ashtakiwa kwa UHAINI
- Mbali na kesi ya Uhaini, Dkt. Malisa afunguliwa pia kesi ya Jinai ya Makosa ya Kimtandao
- Inadaiwa Dkt. Godfrey Malisa ametekwa jana usiku akiwa nyumbani kwake