Aliyetumia chaneli yake katika YouTube kumzushia kifo Dkt. Harrison Mwakyembe, akamatwa

Aliyetumia chaneli yake katika YouTube kumzushia kifo Dkt. Harrison Mwakyembe, akamatwa

Huyo mwakyembe ni nani mpaka azue taharuki kiasi hicho?

Hilo ZEE hata likifa ni sawa tu halina faida zaidi ya kutafuna TOZO ZETU.

Wamuachie huyo dogo. Waache kiherehere.

Kama hawana kazi waje watapishe choo changu hapa kimejaa.
Umaskini umetuletea chuki isiyo na sababu.
Mwakyembe ni raia kama wewe tozo anakulaje?
Afe amekukosea nini?
Wewe unayemtakia kufa una faida gani?
Ukimtakia mwenzio kufa usishangae ukamtangulia kutoa hesabu.
Tusitakiane kufa.
Tutakiane kubadilika yaani kuacha mabaya
 
Atathibitishasha hakumaanisha Harrison huyo pichani
Ifahamike hawa madogo mitandaoni ndio zao,kichwa cha habari kinakushawishi,ukifungua ni utopolo tupu,pengine iwe lesson kwa wenye hizo tabia hasa YouTube imetawala haya maujinga
Kataja jina kabisa
Screenshot_20220926-085035.jpg
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemkamata Tazarn Alfan Mwambengo (27), mkazi wa Ukonga, ambae anatuhumiwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu kifo cha Dkt. Harrison Mwakyembe kupitia chaneli ya televisheni ya mtandaoni jambo ambalo si la kweli.

Katika chaneli hiyo ya mtandao mtuhumiwa huyo aliandika, “BREAKING NEWS HUZUNI YATANDA MAZISHI YA MWAKYEMBE” taarifa ambazo ziliibua taharuki kubwa kwa wananchi hasa kwa Dkt. Mwakyembe mwenyewe na familia yake.
Taarifa za kutafutia viewers😅😅
 
Kwani mwakiyembe s ukoo tu au Dr yeye kajimilikisha Pekee ake

Hiyo kesi nikipewa nashinda kbl bas hazijafika bagamoyo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Watanzania ni wapumbavu sana. Yaan mtu ametaja kabisa Harrison Mwakyembe bado unataka kusema hakumaanisha yy. Hali hiyo mpate maendeleo kwa mawazo hayo ya makalioni.??
 
Nchi hii tumekuwa na watu wa hovyo sana
Siasa zimezalisha kizazi cha ovyo, kizazi kinachopinga kila taarifa za wasio ktk mlengo wao kwa nia ya kudharirisha. Kimezaliwa kizazi ambacho hakioni madhara ya uharifu na waharifu kitawatetea. Uharifu sasa ni ule tu utakaowagusa wao kwa wengine ni uzembe au makosa yao. Sasa hivi Panya road, Wazushi, Majambazi kwa jina la Demokrasia na haki za binadamu wana haki ya kufanya kazi zao. Tuombe 🧎‍♂️🧎‍♂️
 
Wamalizane na Panya Road kwanza hizi mambo za kitaa waachane nazo wakina Mwakyembe wapo wengi...
 
Wanatafuta viewers

Kama yule aliyezusha habari ya mobeyo kujichanganya na siasa

Mpka mwenyewe akakasirika akatoa tamko

Sijui ile ishu iliishia wapi ila mwamba alifuta ile habari [emoji16]
 
Umaskini umetuletea chuki isiyo na sababu.
Mwakyembe ni raia kama wewe tozo anakulaje?
Afe amekukosea nini?
Wewe unayemtakia kufa una faida gani?
Ukimtakia mwenzio kufa usishangae ukamtangulia kutoa hesabu.
Tusitakiane kufa.
Tutakiane kubadilika yaani kuacha mabaya
Wewe ni mke wa mwakyembeh?
 
Hao madogo wa YouTube huwa niwa pumbavu sana,usikute yeye aliandika kabisa Harrison Mwakyembe na kibaya zaidi ukute alitumia hadi picha zake
Haswaa... wanaweka hadi picha halafu mjinga aje kutetea wapuuzi
 
Mbona hizi tarifa uwongo za kufa watu zimejaa sana YouTube [emoji2959]
 
Na hawa inabid wakamatwe pia, kama ndio njia ya kutafuta views sio sawa.Kuna watu uelewa wao mdogo wanaamini kwamba hzo habari zpo sahihi.
 

Attachments

  • Screenshot_20220909-185142_YouTube.jpg
    Screenshot_20220909-185142_YouTube.jpg
    47.1 KB · Views: 1
  • Screenshot_20220922-072653_Instagram.jpg
    Screenshot_20220922-072653_Instagram.jpg
    68.8 KB · Views: 1
Vichannel vya design hivyo viko vingi Sana ...nadhani polisi na TCRA Wana kazi ya kufanya...vinazusha viongozi jinsi walivyokuwa etc..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom