Aliyetumia Silent Ocean - naomba msaada wa ufafanuzi

Aliyetumia Silent Ocean - naomba msaada wa ufafanuzi

herman3

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2015
Posts
556
Reaction score
736
Wapendwa kwa unyenyekevu natanguliza salamu kwenu nyote.

Nimeamua kuanza kununua bidhaa kama mikoba na pochi za wanawake moja kwa moja kutoka China kupitia Alibaba na Aliexpress na kuzileta hapa nikauza, sasa nimeout source baadhi ya supplier kwenye hiyo mitandao na kuona bei zao ni rafiki sana.

Sasa naomba uzoefu kwa mzigo wa milioni moja wa bidhaa hizo gharama za usafiri kupitia Silent Ocean zinaweza kufika kiasi gani? maana nimefuatilia wanasema wanacharge kwa CBM, sasa kwa wazoefu wa kusafirisha bidhaa na hao ndugu naomba japo kujua kadirio la gharama kwa mzigo wa mikoba na pochi wenye thamani ya millioni moja

Ahsanteni

------------------------------------------
Mrejesho

---------------------------------------------------

Ahsanteni sana wadau kwa mchango wenu wa ufafanuzi na uzoefu wenu, nilifanikiwa kusafirisha mzigo wangu wa kwanza kutoka china kwa kuwatumia hao Silent Ocean na hilo lilifanikiwa kutokana na uzoefu ambao mlinishirikisha hapa, na sasa najiona kuwa mfanyabiashara anaye yaelekea mafanikio kwa kuwa nimeanza kufanya hivyo kwa kila bidhaa ambazo wateja wangu wanahitaji.

Mungu awabariki sana
 
Usd 600,cubic meter 1
Ahsante mkuu, ningependa pia kufahamu namna wanavyofungasha mizigo, isije ikawa mzigo mdogo ila ukafungashwa kuchukua space kubwa na charges zikawa kubwa kuliko mzigo wenyewe.
 
Ahsante mkuu, ningependa pia kufahamu namna wanavyofungasha mizigo, isije ikawa mzigo mdogo ila ukafungashwa kuchukua space kubwa na charges zikawa kubwa kuliko mzigo wenyewe
Hapo nenda Instagram kuna page huko watakujibu
 
Wapo vizuri.....
Kwenye CBM inategemea na ukubwa wa Mzigo wako..
Mpe supplier address ya hao majaa aki fikisha mzigo watapima mzigo wako utajua unalipia sh ngap
 
Ahsante mkuu, ningependa pia kufahamu namna wanavyofungasha mizigo, isije ikawa mzigo mdogo ila ukafungashwa kuchukua space kubwa na charges zikawa kubwa kuliko mzigo wenyewe
Mfungasha mizigo ni Supplier wako, wao Silent Ocean wataishia kuipima tu. Inatakiwa Supplier wako akuambie kabla kua mzigo wako una ukubwa gani.

Ili mzigo ukifika Silent Ocean waakuipima Tena ufanye kuhakikisha tu
 
Wapendwa kwa unyenyekevu natanguliza salamu kwenu nyote.

Nimeamua kuanza kununua bidhaa kama mikoba na pochi za wanawake moja kwa moja kutoka China kupitia Alibaba na Aliexpress na kuzileta hapa
Kuna kipindi miakakadhaa nyuma kama minne au mitano niliwahi nunua pochi na viatu kama milion tatu na nusu gharama nilikuja kulipia lak nane na elfu sitini ulipofika yani na kodi umo humo
 
Ahsanteni wakuu, hapo nimeweza kuelewa vizuri sasa, nipo tayari kuendelea katika hatua ya kumlipa supplier.
 
Yes achukue ushauri huu.

Kuongezea Silent Ocean wanacharge USD 450 Per Cubic Meter ya mzigo wako.
Kwa Loose Cargo.

Yan 1m × 1m × 1m kiasi ambacho atatakiwa alipe mzigo ukifika ni USD 450.

AAhakikishe anapata kipimo sahihi cha mzigo wake kutoka wake vinginevyo mzigo utafika bongo atakutana na charges kubwa sana.

All in all, Silent Ocean wako vizuri sana hawana longo longo.
Mfungasha mizigo ni Supplier wako, wao Silent Ocean wataishia kuipima tu. Inatakiwa Supplier wako akuambie kabla kua mzigo wako una ukubwa gani.

Ili mzigo ukifika Silent Ocean waakuipima Tena ufanye kuhakikisha tu
 
Ahsanteni wakuu, hapo nimeweza kuelewa vizuri sasa, nipo tayari kuendelea katika hatua ya kumlipa supplier.
Kabla ya kumlipa supplier wako akuambie kabisa mzigo wako una ukubwa gani, ikiwezekana akupimie uone. Urefu x Upana x Kimo katika vipimo vya mita. Kisha jibu utakalopata katika vipimo vya mita zidisha na hiyo US$ 450 aliotaja mdau hapo juu.

Then utakachopata Kama una afford ndio endelea na mchakato wa kumlipa supplier wako.

Waweza kumwambia pia Kama anaweza kuzibana zaidi Kama hazitopunguza ubora wa bidhaa ili kupunguza ukubwa wa Cubic Meter (CBM).

Kingine cha muhimu inabidi ujue supplier wako yuko mji gani. Maana last time nawatumia Hawa Silent Ocean walikuwepo only YIWU na GUANGZHOU. Sasa ukinunua bidhaa any mji tofauti na hapo then you will be required to pay transportation to those two cities by then. So Kuna ka additional cost hapo jiandae nako pia.
 
Yes achukue ushauri huu.

Kuongezea Silent Ocean wanacharge USD 450 Per Cubic Meter ya mzigo wako.
Kwa Loose Cargo.

Yan 1m × 1m × 1m kiasi ambacho atatakiwa alipe mzigo ukifika ni USD 450.

AAhakikishe anapata kipimo sahihi cha mzigo wake kutoka wake vinginevyo mzigo utafika bongo atakutana na charges kubwa sana.

All in all, Silent Ocean wako vizuri sana hawana longo longo.
Kwa kusema hivyo mfano box langu ni 0.5 x 0.7*0.5 , nitayopata nazidisha mara 450. Kwa uzoefu ako, kuagiza loose cargo moja moja kwa moja ambapo supplier ndo anakutafutia wa kutuma mzigo au kutumia Silent ocean ipi ni nafuu? Na ipi usafirishaji wa mzigo unakuwa wa haraka zaidi?
 
Mfungasha mizigo ni Supplier wako, wao Silent Ocean wataishia kuipima tu. Inatakiwa Supplier wako akuambie kabla kua mzigo wako una ukubwa gani.

Ili mzigo ukifika Silent Ocean waakuipima Tena ufanye kuhakikisha tu
Ni vizuri kabla hujanunua mzigo supplier akwambie huo mzigo utakuwa cubic mita ngapi ukishakua packaged,kama unasafirisha kwa ndege,basi akwambie uzito wa mzigo ili u calculate shipping cost.

Uzuri wa hawa shipping agent gharama zimeinclude import tax,yaani mzigo ukifika wewe unaenda ghalani kwao kulipa na kuchukua mzigo,,hamna urasimu wa kwenda bandarini na makaratasi.
 
Kwa style hio wacha Counsillor Sallah aendeshe Nissan Patrol ya 2020 tu!

Imagine container moja tu lina CBM ngapi? Na jamaa anajazaga Meli 🤣🤣🤣
Ni biashara nzuri sana,mfano wao wanaweza kusafirisha kwa milioni 10,,waka clear mzigo bandarini kwa milioni 20,

Mfano katika container kuna mzigo jumla cubic mita 30,
30*usd600=18,000usd.

Faida ya kutosha tu.
 
wataalamu wanadai usable space ni 28 CBM.

So 28*usd600= 16,800usd.

Roughly wakikuletea waka clear kwa 20M wanabakia na faida ya roughly 10-16M kwa container. Biashara nzuri kweli kweli.
 
wataalamu wanadai usable space ni 28 CBM.

So 28*usd600= 16,800usd.

Roughly wakikuletea waka clear kwa 20M wanabakia na faida ya roughly 10-16M kwa container. Biashara nzuri kweli kweli.
Mwaka 2017 nilisafirisha kwao kwa US$ 350/CBM. Kama ishafika $600 basi mie nikae kimya tu.
 
Back
Top Bottom