Hawahusiki na kukununulia mizigo, ila Alibaba ni sehemu salama kununua mizigo kwa China, kikubwa angalia profile ya supplier wako, soma comments za wateja wengine (kuwa makini pia kuna scammers comments pia), soma specifications za bidhaa unayotaka kununua (picha hudanganya sana ikiwezekana mwambie akutumie video ya bidhaa uione), kama unachukua mzigo mkubwa ni bora ukanunua sample kidogo akutumie ili kuangalia ubora wa bidhaa kabla hujanunua mzigo mkubwa (njia hii imenisaidia sana). Baada ya hapo chat na supplier wako akutengenezee order ya product unayotaka na unampa addrress ya silent ocean, then fanya malipo kwa Alibaba, usilipie nje ya alibaba kwa usalama.
Binafsi transaction zangu za alibaba si nyingi sana ila zimevuka 10M kwa sasa, na sijawahi kupata changamoto yoyote kwa kuzingatia hizo tips ambazo nimekupa.