milele amina
JF-Expert Member
- Aug 16, 2024
- 6,045
- 8,080
Fahamu ukweli wa kesi ya Hamisi Luwongo (Meshack) aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kusabisha mauaji ya aliyekuwa mke wake Naomi Marijani.
Maelezo haya ni kwa mujibu wa maelezo yake akiwa polisi, Mahakamani, Mpwa wake na mjumbe wa nyumba kumi.
Shuka na uzi huu
Image
Tarehe 19 May 2019, Hamisi alienda kituo cha polisi Kigamboni kuripoti kuwa mkewe amepotea huku akieleza kuwa mkewe amepotea tangu tarehe 15 May 2019.
pia akaonesha meseji ambayo alimtumia mke wake siku hiyo:
“mwe simu yangu iliibiwa nimeipata nahisi hao vijana wako, then nakupa taarifa leo ya ngap hulali nyumban muda sasa, sasa nakupa taharifa mm naondoka mtoto namwacha nyumbani peke yake na kesho nasafir naenda nje ya Tanzania sasa ww kaa na vimalaya vyako vya hovyo mimi nina mtu mwenye pesa sio ww kiruka nj …Na hutonipata tena kwa namba hii…be responsible kulea mtoto”.
Miezi miwili baadae polisi walifanya uchungzi wakagundua kuwa meseji iliyooneshwa na Hamisi inaoneakana illitumwa katika same location wakapata wasiwasi ndipo tarehe 16 July 2019 Kituo kikuu cha polisi Dsm kilimuita Hamisi na kufanya nae Mahojiano.
Hamisi alikubali kusababisha kifo cha mke wake na anasimulia katika maelezo ya onyo kama ifuatavyo:
Tarehe 14/05/2019 mimi nililala nyumbani kwa MAGRETI kulikokucha asubuhi majira ya saa 07:00 ndio mimi nilirudi nyumbani kwangu hio ni tarehe 15/5/2019 nilivyorudi nyumbani nilumkuta mke wangu NAOMI anamuandaa mtoto wetu kwenda shule, hivyo mimi nilimpita tu na kuingia ndani na mtoto alichukuliwa na pikipiki kwenda shuleni.
...Baada ya mtoto wetu kwenda shule simu yangu iliita kwa jina la mwanamke huyo Magreth hivyo alivyoona hivyo alianza kunitukana mimi nilimwambia wewe chukua unachokitaka uondoke kwani hakuna ndoa tena hapa muda wote wa miaka miwili mimi na wewe tunalala kila mtu kitanda na chumba chake hunijui na mimi sikujui kwa hio sioni sababu ya kurumbana hivyo ugomvi wa kutukanana
ukawa mkubwa hapo ndani kwetu, na hapakuwa na mtu yeyote, wakati huo mimi sikuwa nimevua nguo ambazo nimekuja nazo na yeye alikuwa amevaa nguo ya ndani na kanga mbili hivyo tulianza kupigana,
na nyumba yetu ina kigorofa chumba changu kipo juu chake kipo chini hivyo ili kufika chumbani kwangu lazima kupitia chumbani kwake hivyo ugomvi huo ulitokea chumbani kwake, hivyo tulipigana kwa ngumi bila silaha ya aina yeyote.
... huyo mwanamke alikuja na kunivuta mapumbu hivyo mimi niliamua kumsukumia na kudondokea kichwa kwenye mlango wa chooni na baadae
alijipiga chini akawa anatoka damu nyingi puani na mdomoni, wakati anaendelea kugaragara akawa anasema Mungu amsamehe na hakunyanyuka pale chini alianza kukoroma na baadae alifariki dunia hapo hapo....
nilikwenda kufunga geti la nje ili kufikiria cha kufanya, jambo la kwanza ni kujua wapi nitaupeleka mwili wa marehemu na namna ya kutoa taarifa ya tukio hili kwa ndugu na familia...
Nikajiuliza maswali mengi kama nitambeba kwenye gari huu mwili nikikutana na trafiki njiani sina cha kusema au nikiutoa usiku kama ninakutana na askari wa doria sina kitu cha kuwaeleza.
Jambo lingine nikawa kuuzika hapo ndani nikaogopa watu wakija, kufukua wakapata ushahidi dhidi yangu hivyo nikaamua kuuchoma moto hapo nyumbani isipokuwa nisitumie kuni kwani zitakuwa nyingi Sana hivyo niliamua kutumia mkaa.
Nikakumbuka kwenye banda la kuku nilikuwa nimechimba shimo kusudi maji machafu ambayo wanaoshea vyombo yaingie humo badala ya kusambaa hivyo nilichukua sululu na kwenda kongeza hilo shimo na pia nilihakikisha milango yote nimefunga kwa ndani mtu hawezi kuingia.
Mara baada ya kumaliza kuandaa shimo niliingia ndani na kuukunja huo mwili kwenye mashuka mawili kisha nikauburuza kupitia mlango wa jikoni hadi kwenye shimo hilo ukazama wote kichwa kikiwa juu kama amekaa.
Hapo nilimpigia Thomasi kijana wa boda boda akaleta mafuta ya taa lita tano, nikampokelea hapo getini hakuingia ndani nilimpigia Adeliki akaleta magunia mawili ya mkaa nilimwambia achague mkaa mzuri alivyoleta nilimpokelea hapo getini na yeye hakuingia ndani.
Nilivyo kwisha kamilisha vyote ndio mlianza kuuchoma mwili kwa moto Nilitumia pia viatu vibovu ambavyo vilikuwa nje kwani nikiweka mafuta ya taa mafuta yana waka mara moja ila viatu vinachukua muda hivyo vilisaidia Sana hata moshi uiikuwa unatoka ule wa viatu na hakuna harufu kutokana
na viatu hivyo baada ya moto kuendelea kuwaka nilikaa kwenye kibanda changu ikawa naenda kuongeza mkaa na kuugeuza mwili kusaidia uweze kuungua vizuri Hakuna mtu yeyote ambaye mimi nilisaidiana nae maana moyo wangu ulikufa ganzi nikajua hili la kwangu mwenyewe ndio maana
nilichoma kutokuwa na ushahidi popote na nilichimba shimo kusudi moto huo usisambae na kuungua kiurahisi Nina kumbuka kwani kama saa 11 ndio mlianza kuchoma hadi mwanagu anarudishwa kutoka shuleni bado nilikuwa na choma hapo tayari kila kitu kimekwisha ni moto tu kuzimika... hadi saa 15:00 au kumi kila kitu kimekwisha bado vichenga chenga vya mkaa...
Tarehe 16/05/2019 saa 06:00 nilichota majivu na kupakia kwenye gari kupelekea kutupa shambani kwetu ambapo nilibeba kwenye kiroba ambacho kilikuwa nyumbani kimeisha unga.
Hivyo mimi kwenda hadi shambani kwetu mbele ya Mwasonga vyote nilibeba kwenye gari yangu aina ya Subaru.Nilivyofika hapo shambani nilichimba shimo la mgomba nikamimina yale majivu halafu nilipanda mgomba, na mgomba mwingine sikupanda kwa hayo majivu, baada ya kumaliza nilirudi nyumbani.
Niliamua kuchota hayo majivu kupeleka shambani kwani nilijua kwamba kama majivu hayo yatakutwa pale yatachunguzwa japo nilipeleka huko lakini vipande vya mabaki haviwezi kukosekana lile shimo ambapo nilimchomea Naomi pale nyumba
nililichimba zaidi na kujaza kifusi na mafundi wangu ndio walioendeleza pakiwa hakuna mabaki na baadae mimi nilijaza kifusi na kupiga floor na huwezi kulifahamu hilo eneo tena.
Wakati mwili wa Naomi unaendelea kuungua nilichukua line za Naomi na kuweka kwenye simu yangu na kujitumia sms kwenye simu yangu kuwa naenda nje ya nchi
hutaniona tena, wala kupatikana kwa line hii na nikasema endelea kubaki na vimalaya vyako meseji ambayo nilituma kwa ndugu zake kuonesha nimetumiwa na Naomi jambo ambalo nilikuwa najihami kwa ndugu na mkono wa sheria…
Tarehe 17/05/2019 mimi nikiwa hapo nyumbani nilichukua line nyingine ya Naomi nikajitumia sms tena kwamba niwe responsible kulea mtoto,...
Jumamosi tarehe 18/5/2019 natumaini ndio nilienda kutoa taarifa kituo cha Polisi pia kwa ndugu zake hivyo polisi walinipa RB wao kuendelea na uchunguzi mimi taarifa hiyo mlitoa kituo cha Kigamboni
isipokuwa ndugu wa Marehemu wao walienda kutoa taarifa huko Temeke.Kwa muda wote huo sikuwahi kusema ukweli huu hadi leo hii tarehe 16/07/2019 nikiwa kituo cha Polisi cha Centro ndio nimeamua kutoa ukweli huu juu ya kifo cha Naomi na kwamba hadi muda huu mimi nipo tayari kuwapeleka nyumbani kwangu Kigamboni.
kuonesha sehemu ambayo nimemchomea pia kuwapelekea huko shambani kwetu kuonesha sehemu ambayo mimi mlimwaga majivu ya Naomi ambaye nilimua kutokana na ugomvi huo ambao hata wazazi walikuwa wanafahamu migogoro yetu kwenye mapenzi.
Baada ya kutoa maelezo hayo ya onyo Polisi walienda nyumbani kwake na kukuta mifupa na meno ambayo baada ya vipimo ilijulikana ni vya mwanamke then baadae wakamchukua hadi kwa kiongozi wa mtaa na alikriri then wakamfungulia kesi ya mauaji.
Jamaa alipofika mahakamani alikataa kuua na alieleza kuwa aliandika maelezo ya onyo ya uongo kuogopa kuteswa lakini hakuua wala kufanya aliyoyaeleza
upande wa mshiataka ulileta mashahidi 14 na kati ya hao mashaidi alikuwa mpwa wake ambae alisema mbele ya mahakama kuwa Hamisi alikiri mbele ya balozi na yeye akiwemo kumuaa mke wake naomi.
Pia walipoenda shambani walikuta majivu ambayo Hamisi aliyachimbia chini, pia polisi walivyoenda kwenye Ghorofa ya Hamisi mbele ya kitanda kulikuwa na mabaki ya damu walipopima waligundua kuwa damu ya mwanamke.
Hamisi alikubali kukutwa na Sim Card za mke wake hivyo ilihashiria kuwa jamaa alijitumia sms vilevile kitendo cha kuanguka mkewe bila kujali na baada ya kufa kumchoma moto na kwenda kutupa majivu shambani ilionesha ana nia kuua hivyo mahakama ikamuhukumu kunyongwa hadi kufa.
MWisho