Aliyewahi kuagiza Alibaba au anajua office zao zilipo kwa Dar

Yea, yani hujawahi pambana na shipping za Singapore wala Caniao miezi 3 [emoji3][emoji3], hujapigiwa simu posta, hujaona tracking inakwambia mzigo uko held na custom uende direct ku bargain na supplier Alibaba[emoji1] akomae Kwanza huko
Uko sahihi mkuu
 
Watumia mfumo gani kupokelea vitu???
 
Wasi wasi wangu ni kwamba unaweza purchase kitu cha bei kubwa ikitokea longo longo unamfata nani maana kwa kuchat tu na mtu haitoshi
kuna guarantee, usipopokea ulichoangiza raise dispute utarudishiwa pesa yako. Next time jaribu ebay au amazon na avoid suppliers from China
 
Asante kwa kuwa umeanzia kikuu. Njoo AliExpress then Alibaba.
Mimi bado nipo AliExpress.
Ila kwa uhakika na uharaka tumia private shipping kama ocean au unique air
 
Hamna ofisi zao Dar ila unapokea kwa shipping agent. Mimi nilikuwa natumia Silent Ocean. Unasema mzigo utumwe Guangzhou kwa china kwenye address ya Silent Ocean. Mzigo ukiwafikia Silent watautuma Dar unaenda kuchukua pale kwenye Godown lao la karibu na Keko. Safety kwa Silent Ocean iko vizuri nimeshafanya biashara nao za 10s of millions. Changamoto ambayo ni kuhakikisha hukosei ni kuchagua supplier mzuri kwenye Alibaba.
 
Nieleweshe vizuri kuhusu Silent Ocean na jinsi ya kuwapata
 
Asante kwa kuwa umeanzia kikuu. Njoo AliExpress then Alibaba.
Mimi bado nipo AliExpress.
Ila kwa uhakika na uharaka tumia private shipping kama ocean au unique air
Nieleweshe kuhusu hao agents kupitia AliExpress
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] wadau wanapenda
Kitonga dhaaaa
 
Safety kwa Silent Ocean iko vizuri nimeshafanya biashara nao za 10s of millions.
Nasikia hawa jamaa wanachelewesha sana mizigo hili nalo ni tatizo miezi mpaka mitatu mzigo haujafika
 
Mkuu kua makini sana. Kuna jamaa yangu hivyo hivyo alihamishia mazungumzo private, na akawa anaagiza mizigo fresh inakuja mpaka akajenga uaminifu kabisa akawa anaagiza mizigo mikubwa fresh tu. Kumbe analiwa mingo, mara ya mwisho kaagiza mzigo wa 200m+ mtu kapotea hewani mazima. Jamaa kaenda mpaka China lakini wapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…