Aliyewahi kuagiza Alibaba au anajua office zao zilipo kwa Dar

Aliyewahi kuagiza Alibaba au anajua office zao zilipo kwa Dar

Mkuu kua makini sana. Kuna jamaa yangu hivyo hivyo alihamishia mazungumzo private, na akawa anaagiza mizigo fresh inakuja mpaka akajenga uaminifu kabisa akawa anaagiza mizigo mikubwa fresh tu. Kumbe analiwa mingo, mara ya mwisho kaagiza mzigo wa 200m+ mtu kapotea hewani mazima. Jamaa kaenda mpaka China lakini wapi.

Story tatu
 
Alibaba na Aliexpress ni waaminifu sana, huwa hawaachii hela kwa supplier mpaka wewe ukubali kwamba umepokea mzigo wako. Na usipopokea unafungua dispute ambapo baada ya siku 21 za kazi hela yako inarudi yote. Namna ya kupokea mzigo wako ni kupitia posta. Taadhari ukishalipia mzigo ukaona supplier hajafanya shipping ndani ya siku 7 anza kumbana, mawasiliano yote yafanyike kupitia platform ya ALIBABA usikubali mawasiliano kwa njia ya email.
Huwa wanataka kuchat WhatsApp aisee Mimi naogopa kisa hicho tu
 
Wadau naombeni nisiwe na mambo mengi naombeni kujua yeyote aliyewahi agizia mzigo Alibaba ulimfikia vipi na ofisi za agent zao hapa Dar zipo wapi?

Mimi nina experience na Kikuu nimeagiza sana na kupokea mizigo yangu mara ya mwisho nilinunua mzigo wa Million 1,200,000/= nilifanya maana ofisi zao nilienda pale Shoppers plaza msasani so nikawa confident kikitokea chochote ninao wa kukabana nao.

Natamani Alibaba wana vitu vingi na cheap zaidi ya Kikuu.
Alibaba hawa Ofisi Bongo. Period.

Kama unasubiri wawe ofisi ndio ufanye nao biashara endelea kusubiria.
 
Wasi wasi wangu ni kwamba unaweza purchase kitu cha bei kubwa ikitokea longo longo unamfata nani maana kwa kuchat tu na mtu haitoshi
Fatilia mambo mzee... Haya mambo ya kupigizana kelele na mtu yameshapitwa na wakati.

As long as umefata procedures zote. Hakuna mtu wa kukutapeli hela zako kwenye platform zote kubwa za kibiashara.

Ebay, Amazon, Alibaba, Aliexpress, Taobab, 1688 n.k.
 
Halafu pia,
Mimi nina mdogo wangu Yuko Guangzhou ana shipping company yake hivyo nachofanyaga nikishamalizana na jamaa wa Alibaba wanapeleka mzigo kwake halafu yeye ndio namtumia kunitumia mzigo
 
Mini ninanunua bidhaa alibaba na aliexpress kuleta UAE
Wako wengine kama wish.com, Mama.com, Dhgate, wish na mama ni retail lakini wana matatizo kwenye shipping, wakati mwengine hupati mzigo lakini wako haraka kurudisha fedha kama hukupata mzigo. DHgate zaidi wako kwenye wholesale na service zao ni bora zaidi.
Tafauti na alibaba hizi site nyengine hawana direct chat kama alibaba, mara nyingi unapatata fununu yupi seller/ manufacturer mzuri wakati wa kuchat ambapo unatoa duku duku zako zote.

Usafiri kutoka china to AmUAE unachukua 7-14 days kwa ndege na kwa bahari ni 21-30days.
Mimi natumia agent ambaye ana office china na uae
Ni vizuri kuwa na shipping agent ambaye yuko china kwa sababu akipokea mzigo tu, una hakika utaupata mzigo wako na anaweza kukusaidia kwa inspection kabla ya shipping.

Naweza kusema kwa miaka mitano ninanunuwa mzigo alibaba sijawahi kupata matatizo yeyote.
Nimefikia Gold status, hii status ukiifikia unapata majibu haraka kwa suppliers na benefits nyengine na suppliers wengine wanakutafuta.
 
Tafauti na alibaba hizi site nyengine hawana direct chat kama alibaba, mara nyingi unapatata fununu yupi seller/ manufacturer mzuri wakati wa kuchat ambapo unatoa duku duku zako zote.
Mkuu hapa ungedadavua kwa utuo ingependeza mkuu kama hutojari
 
Nimefikia Gold status, hii status ukiifikia unapata majibu haraka kwa suppliers na benefits nyengine na suppliers wengine wanakutafuta.
Gold status unaifikia kwa vigezo gani na ni benefits zipi wanatoa baada ya kufikia hapo?
 
Niliwapata ila hawajibu message nikaachana nao,

Nawatumia Kikuu hawajawahi niangusha tatizo lao hawana bidhaa nyingi kama Aliexpress, basi nakerekaaaaa

Naam, kikuu wana bidhaa chache sana na hata zilizopo unajipata hakuna choices tofauti tofauti...
 
Niliwapata ila hawajibu message nikaachana nao,

Nawatumia Kikuu hawajawahi niangusha tatizo lao hawana bidhaa nyingi kama Aliexpress, basi nakerekaaaaa
Tumia aliexpress wana mazaga kibao bei chee nina mizigo yangu mitatu from Aliexpress naisubiri mmoja umeshafika bongo miwili bado

Sent from my TECNO-L8Plus using JamiiForums mobile app
 
Ila bei za mi actual au ni mambo yao ya kichinachina mizingua
 
Mchawi ni hilo sanduku la Posta,
Au wewe wapokelea vipi mizigo yako
Mi sina sanduku la posta na haina ulazima kuwa nalo ukiwa Kwenye profile yako utajaza shipping address ambayo ni jina lako, sehemu uliyopo utajaza nchi Tanzania,mkoa wako,zipcode pamoja na namba yako ya simu ili mzigo wako ukifika utapigiwa simu na posta(Mizigo inapelekwa posta ikifika bongo)

Hiyo picha hapo chini ni address yangu

Screenshot_2022-06-10-20-23-14.jpg


Sent from my TECNO-L8Plus using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom