TANZIA Aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa mbalimbali nchini, Abass Kandoro afariki dunia Hospitali ya Taifa, Muhimbili

TANZIA Aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa mbalimbali nchini, Abass Kandoro afariki dunia Hospitali ya Taifa, Muhimbili

Imethibitishwa Abass Kandoro hatunaye tena. Source inasema alikuwa ICU kwa muda mrefu sana.

Kandoro amewahi kuwa katika nafasi ya ukuu wa Mkoa katika zaidi ya Mikoa Sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Singida na Mbeya.

Abbas%2BKandoro.JPG
Lo ,masikini kaka yangu Abbas Kandoro.
Alikuwa mtu mwadilifu sana, hakuwa na mizaha mizaha kazini.
Na alimsikiliza kila mtu, na hakuwa mtu wa makuu.
Kitaaluma alikuwa economist, na kwenye planning alikuwa vizuri sana.

Majuzi wiki iliyopita, nikitoka Mbeya, pale karibu na Ifunda , Iringa, nyumbani kwao,nikawakumbusha wenzangu kwenye gari kuwa pale ndio kwao Abbas Kandoro, aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa ya DSM , Mbeya Mwanza n.k.
He led a simple life.

RIP Abbas Kandoro
 
HAKIKA SISI NI WA MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA...

MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI... AMEN
 
R.I.P mzee wetu, umetuachia maji ya kandoro si haba, tutakukumbuka.
 
Mbele wewe nyuma sisi, zamani walikuwa watawala bwana tofauti na sasa.
 
Tangu nimeanza kujielewa na kufuatilia mambo mbalimbali ya kidunia, huyu ni kati ya wachache ambao kwa maoni yangu wamehudumu nafasi hiyo kiasi kwamba unaweza kujustify uwepo wa nafasi ya mkuu wa mkoa. Busara mingi, very charismatic.
Wengine ni:
Parseko Kone
Steven Mashishanga
Phillip Mangula
Tarimo
Meja Balele
Eng. J. Nsekela
Mkuu wa mkoa wa sasa wa Kagera.
Na Godfrey wa Lindi anaelekea elekea.
Uongozi unaonekana machoni mwao hata kabla hawajaongea. Wamebarikiwa busara sana.
Apumzike kwa Amani Abbas Kandoro.
 
Kandoro amewahi kuwa katika nafasi ya ukuu wa Mkoa katika zaidi ya Mikoa Sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Singida na Mbeya.

Umeshindwa kumalizia kutaja mikoa miwili tu!!?
 
Back
Top Bottom