Masikini_Jeuri
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 6,829
- 1,303
Swali: jamii na serikali tunaleaje vipaji kama hivi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
![]()
MWANAFUNZI aliyeongoza mtihani wa kidato cha nne kitaifa mwaka 2010, Lucylight Mallya (18), amebainika kuwa ni yatima ambaye wazazi wake wote walifariki dunia miaka minne iliyopita.
Halafu bado tunawazia mambo ya viti maalum kwa wanawake, wakati kwa hali inavyoonyesha viti maalum kwa siku za usoni zitatakiwa kupewa akina baba!..huh!
Alaaaa kumbe wameanzisha na ya wavulana safi sanaHongera binti.
Marian wameanzisha Marian boys huenda ndo sasa ikaja ikawa kinara wa shule za sekondari hapa nchini
Na asizisikie kabisaMungu ampishie m,bali habari za siasa tena za bongo?
Binafsi nampongeza huyu Binti, kama kweli pamoja na kutokuwa na wazazi wake amefanya hivi basi iwe changamoto kwa Yatima wengine na wote, kufiwa na wazazi kuna huzunisha ila isiwe kigezo cha kutaka kuhurumiwa tu, juhudi ni kazi na kushirikiana na walezi wengine mtu yoyote atafanikiwa na Mungu ni mwema.
hongera sana dada, ila tatizo la kina dada zetu wengi wakifika hatua ya chuo wanapwaya....
PP, umeibua hoja nzuri pia, hii ya baadhi ya wanafunzi (wavulana na wasichana) kufanya vizuri shuleni (oleve & Alevel) lakini wakifika vyuoni shule inwatesa sana..wanastruggle kweli mpaka unashangaa hivi ni mtu yule yule ambaye cheti chake cha form six kinaonesha ametapa div 1 ya point 3!
Mimi nadhani ni baadhi ya shule/walimu kuwadekeza sana wanafunzi katika ufundishaji...kwa msemo kimombo tungesema 'spoon feeding'. Kwa mtizamo wangu, wanafunzi walipitia kwenye shule ambazo walikuwa wanakuwa spoon fed, wakifika vyuoni wanapata tabu.
Hongera binti.
Marian wameanzisha Marian boys huenda ndo sasa ikaja ikawa kinara wa shule za sekondari hapa nchini