Superman
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 5,693
- 1,702
![]()
MWANAFUNZI aliyeongoza mtihani wa kidato cha nne kitaifa mwaka 2010, Lucylight Mallya (18), amebainika kuwa ni yatima ambaye wazazi wake wote walifariki dunia miaka minne iliyopita.
Ruta;
Asante sana this is very inspiring and we should be proud of gals like her.
Wanaharakati wa Maendeleo ya wanawake ni vema wakalichkua zaidi na kulitumia katika kudai usawa wa kijinsia kuwa "WANAWAKE WAKIPEWA NAFASI WANAWEZA"
Hata hivyo nitoe angalizo kuwa Elimu pekee si mafanikio katika Maisha. Inahitaji jitihada ya ziada katika maeneo mengine. Nina mifano ya watu wengi walioanza maisha mara tu baada ya kumaliza darasa la saba au form IV lakini sasa wana maendeleo makubwa sana kutokana na juhudi zao halali.
Tunayo pia mifano ya watu wengi ambao wamekuwa wakiongoza kimasomo la saba, O-level, A-level, University lakini maisha hayaendi sawa.
Sina maana kuwa Elimu isizingatiwe na si kwamba haina mchango katika maisha, lakini yataka jitihada ya ziada kufanikiwa katika maisha.
QED