Aliyoyasema Abdul Nondo akiwa kwenye mkutano wa Baraza La Vijana la CHADEMA (BAVICHA)

Aliyoyasema Abdul Nondo akiwa kwenye mkutano wa Baraza La Vijana la CHADEMA (BAVICHA)

Kama Kikwete alipogombea uchaguzi wa 2005 alikuwa anaitwa kijana akiwa na 54yrs, huyu Nondo huko ccm kwa umri huo si atachukuliwa kama ananyonya?
That's not a scholarly answer. It's like that from CCM about Kikwete! Ahahahahaha!!
 
Wakuu,

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo, Abdul Nondo, Nondo wakati akitoa salamu za ngome hiyo katika mkutano wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) unaoendelea katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo Jumatatu, Januari 13, 2025 amesema:

“Sisi vijana wa vyama hivi tuna ajenda zinazofanana na changamoto zinazotufanya tuungane. Changamoto za kidemokrasia, kama vile kuvurugwa kwa uchaguzi, zinaathiri wote bila kujali itikadi zetu,” amesema Nondo.

Akitilia mkazo suala la usalama wa vijana, Nondo ameeleza vitendo vya kutekwa kwa baadhi ya watu vinapaswa kufika mwisho.

“Inawezekana tukawa tunatofautiana katika mambo madogo, lakini mambo makubwa yanayotuunganisha ni muhimu zaidi. Lazima tuunganishe nguvu kwa ajili ya usalama wetu.”

Pia ametoa wito kwa wale watakaochaguliwa katika nafasi mbalimbali kuhakikisha wanachukua hatua za kuzuia vitendo vya utekaji, akisema: “Haya mambo ya kutekwa lazima yafike mwisho,” amesema


View attachment 3200804

Gen Z wanaanza kuamka. Nimemsikia wa Cuf naye anaongea hivyo hivyo. Sasa hawa vijana wakiacha kuwasikiliza Wazee hasa wa kizazi chetu tuliochakachuliwa JKT watalikomboa taifa toka kwa Mkoloni mweusi.
 
Back
Top Bottom