Aliyoyasema Amri Kiemba ni madai mazito na hatari kwa soka letu, yachunguzwe

Aliyoyasema Amri Kiemba ni madai mazito na hatari kwa soka letu, yachunguzwe

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
Jana saa tatu usiku katika kipindi cha Sports Roundup kinachorushwa na Clouds FM, mchezaji wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga ambaye siku hizi ni mchambuzi wa soka, Amri Kiemba alitoa madai mazito, ya kushtusha na yenye sura ya kijinai yanayoendelea kwenye soka letu

Kiemba alisema makocha wanaopewa kazi ya kusajili wachezaji kwenye vilabu vingi vya madaraja ya juu wanachukua kwa siri na kwa ubabe kinachoitwa commission kutoka kwenye ada za usajili za wachezaji wanaosajiliwa nao

Zaidi ya hapo alisema pia hata wachezaji husika wanapokua wamesajiliwa Makocha huchua asilimia fulani kutoka kwenye mshahara yao ili waendelee kubakia kwenye club vinginevyo wakikataa hufanyiwa zengwe na figisufigisu kwa kuwekwa bench, kufanyiwa kampeni za kuwachafua na hata kuachwa kwenye sajili zinazofuata

Muongoza kipindi Alex Luambano alipomuuliza labda pengine suala hilo lipo kwa baadhi ya vilabu, Kiemba alikataa na akasema kwamba club na waalimu wenye mtindo huo ndio wengi zaidi kuliko ambao hawafanyi hivyo!!!!

Amri Kiemba ni mdau wa michezo na alikua mchezaji wa ligi kuu na timu ya Taifa. Kwahiyo ana uhakika wa anachokisema hasa ukizingatia madai yake kayatoa hadharani kwenye chombo rasmi na kikubwa cha habari

Natoa wito kwa mamlaka husika za soka na za uchunguzi wa jinai nchini zifanyie kazi madai haya mazito ambayo kama ni ya kweli basi ni tatizo kubwa na ni uhalifu dhidi ya vijana wetu. Jambo hilo inawezekana likawa miongoni mwa vyanzo vya kufifisha juhudi za vijana kupata maendeleo kwenye soka na kuishia kucheza mpira mchangani tu na kurudisha nyuma maendeleo ya soka letu
 
AMRI KIEMBA HAFAI HATA KUCHAMBUA MCHEZO WA REDE.
Inamaana haya sio madai ya kweli? Kama aliyeyatoa ana akili timamu na kayatoa live kwenye chombo cha habari kwanini uchunguzi usianzie kwake aweze kutoa taarifa zaidi? Vinginevyo uongozi wa Clouds FM utoke mbele na kujitenga na madai hayo mazito
 
Sasa Kama wanataka connection kwa nini wasikatwe commission na maconnector
Commission inaweza kuelezeka, lakini commission kwenye mshahara HAPANA!!! Tena alisema unaweza kuta kocha anawachezaji wake sita kila mwisho wa mwezi anakinga mkono kupokea pesa. Sasa kama ni halali kwanini wafiche? Na mchezaji anapokataa anafanyiwa figisu
 
Mbona hilo linajulikana,hivi unamuchaje mchezaji kama Rashid Juma au unamuacha Paul Bundala unamsajili Kennedy Juma,jibu ni rahisi tu ni Commission wanayopata wanaosajiri...eti Simba inamsajili Charles Ilamfya,si vichekesho hivyo.
 
Kuna shida kubwa kwenye mfumo wetu wa uendeshaji soka, uibuaji vipaji na usajili wa wachezaji
 
Mbona Kennedy na Ilamfya ni wachezaji wazuri tu! Kukaa bench kunatokana na kuwapo kwa wazuri zaidi katika nafasi zao. Paul Bundala na Rashid Juma nao walikuwa wanakaa benchi hivyo hivyo, sasa ni heri wakacheze sehemu nyingine. Wakati mwingine tupunguze kulaumu laumu, hivi Ilamfya atatoa commission gani ili Kishingo amsajili?
 
Kuna shida kubwa kwenye mfumo wetu wa uendeshaji soka, uibuaji vipaji na usajili wa wachezaji
Ni kweli kabisa ni uhuni unafanyika sana kwenye soka...yaani unakuta mchezaji super star anacheza club kubwa lakini maisha yake ya kawaida au ya chini tu...kumbe kuna pimbi kibao zina share mshahara na hela za usajili za wachezaji.
Kuna siku nimekaa mazoezini nasikia watu wanamsifia Shabalala kwamba maisha yake mazuri...wamemuona Goba Center ananunua matunda akiwa na Crown mpya nyeusi...sasa unajiuliza kwa jina la zimbwe lilivyo mchezaji wa kutegemewa wa Simba na Stars...kweli Crown ni gari ya kusifiwa nayo na kuonekana ameyapatia...tunakutana na kina Mlipili,Joseph Mahundi nk mazoezini lakini zaidi ya uzoefu wao wa kucheza premier,maisha yao ni kawaida sana ...hawa watu ni wanaibiwa sana na hakuna wa kuwatetea.
 
Mbona Kennedy na Ilamfya ni wachezaji wazuri tu! Kukaa bench kunatokana na kuwapo kwa wazuri zaidi katika nafasi zao. Paul Bundala na Rashid Juma nao walikuwa wanakaa benchi hivyo hivyo, sasa ni heri wakacheze sehemu nyingine. Wakati mwingine tupunguze kulaumu laumu, hivi Ilamfya atatoa commission gani ili Kishingo amsajili?
Mkuu hujanielewa kilichomaanisha labda.

Paul Bundala na Kennedy Juma uwezo wao haupishani...ila usajili unafanyika ili kuwe na chances za kupata commission kwenye hela ya usajili na hata mshahara yaani inategemea tu.

Kuhusu Ilanfya kila mtu anajua pale hawezi cheza...atazugazuga tu baadaye atatolewa kwa mkopo na kuishia hukohuko.

Kuhusu commission zinaliwa zaidi na wahuni kuliko hao makocha...na makocha wenyewe siyo level za kina Kishingo.
 
Mkuu hujanielewa kilichomaanisha labda.

Paul Bundala na Kennedy Juma uwezo wao haupishani...ila usajili unafanyika ili kuwe na chances za kupata commission kwenye hela ya usajili na hata mshahara yaani inategemea tu.

Kuhusu Ilanfya kila mtu anajua pale hawezi cheza...atazugazuga tu baadaye atatolewa kwa mkopo na kuishia hukohuko...commission zinahusika sana tu.

Kuhusu commission zinaliwa zaidi na wahuni kuliko hao makocha...na makocha wenyewe siyo level za kina Kishingo.
 
Yule GK Mtoto wa Manzese alieibukia Morogoro... baadae SIMBA... baadae tena COASTAL UNION... usajili wake ulikuwa km anavosema KIEMBA... akagoma kutoa COMMISSION... aliemsajili akamuapiza TUTAONA KM UTADAKIA SIMBA... kilichofuata ni History

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Ni wengi tu...tena kabla hujasajiliwa unaambiwa kabisa..ukikubali ndo wanakuchukua ukigoma utabaki hukohuko...labda uwe na kipaji kikubwa sana.
 
Kiemba asipuuzwe hata kidg anachokisema inawezekana tatizo ni kubwa kuliko hata tunavyofikiri pia aliwahi kusema kuhusu timu ya taifa kwamba ukiitwa timu ya taifa usipotoa Asilimia fulani ya posho utakazopata huko hautakaa uitwe tena tena pesa hizo zinapokelewa pale TFF hiyo ni kuanzia kocha mpaka wachezaji.
 
Back
Top Bottom