Aliyoyasema Amri Kiemba ni madai mazito na hatari kwa soka letu, yachunguzwe

Kuna Dogo langu alikuwa sehemu ya kikosi kuipandisha timu ligi kuu last year...walivyopanda na mkataba wake ulikua umeisha katika kuurenenew Dogo aliambiwa mshahara utakuwa pasu kwa pasu na kocha yaani 50% na 50% kwa kocha yupo mtaani anagonga ndondo na analisha mke na mtoto wake mmoja ..Dogo ana 22 years umri wa mpira
 
Huu ni uhalifu kwenye mpira lazima vitendo hivi vipigwe vita. Hatua ya kwanza ni kwa wadau wote wa soka ikiwemo mashabiki wapaze sauti. Hii itasaidia wenye michongo hiyo kuona aibu na kuacha maramoja
 
bro una hasira kwelikweli,umekula lakini au ni njaakalihatari?
 
Huu ni uhalifu kwenye mpira lazima vitendo hivi vipigwe vita. Hatua ya kwanza ni kwa wadau wote wa soka ikiwemo mashabiki wapaze sauti. Hii itasaidia wenye michongo hiyo kuona aibu na kuacha maramoja
Mtu wa kwanza ni Jamhuri Kihwelu Julio.

Zamani walikuwepo wakina kabourou na Hans pope wa simba. Ndio mishe zao hapa mjini. Wapo wengi sana
 
Alichokisema Kiemba ni ukweli mtupu

Hata Charles Ilanfya alishazungumza hayo kipindi akiwa KMC.
Alifuatwa na kiongozi mmoja wa Yanga akamwambia ntakufanyia mpango usaini Jangwani kwa dau la 20ml lakn utanimegea 10ml na inayobaki ni ya kwako,,Charles akakataa, dili ikafa.
 
Kirusi kikuu cha huu uhuni ni TFF, just imagine timu za mikoani zinapambana kutafuta vyanzo vya kulipa mishahara wachezaji, alafu TFF wanakula zawad yao tena wanatoa sababu za kipuuzi eti kuna wachezaji wa kigeni walikuwa wanadaiwa signing fee, mara imebaki million 1! Kwenye mpira wa miguu tuna viongozi wabinafsi, wahuni, wala rushwa, nadhan Magufuli aanzie TFF kama anataka timu bora ya Taifa.
 
kidau na karia ni janjajanja na haihitaji uwe profesa kuwajua kuwa hawa ni wasanii, wahuni nk.
 
Hao TFF wajinga sana. Timu za vijana Hakuna mtoto anaweza kuitwa bila kuhonga.


Nina mdogo wangu anachezea Timu ya vijana katika moja ya timu zibazoshiriki VPL, nilikutana na makocha wa timu ya taifa wakanichana live niwahonge ili aitwe under 17 National team. Tff ni uozo mtupu. Watu wanaitwa sio kwa vipaji vyao ila kuhonga.
 
Sasa nimepata jibu kwanini soka letu halipigi hatua! Utashangaa kuona kwenye mechi za mchangani za vijana kuna vipaji vya hali ya juu sana lakini ukija kwenye timu za taifa za vijana huoni hivyo vipaji!
 
Sasa nimepata jibu kwanini soka letu halipigi hatua! Utashangaa kuona kwenye mechi za mchangani za vijana kuna vipaji vya hali ya juu sana lakini ukija kwenye timu za taifa za vijana huoni hivyo vipaji!
Ndio Siri hiyo nimekupa na Kama wanapita humu wathubutu kubisha tumwage mboga.

Mpira wa bongo Ni magumashi wachezaji wananyonywa sana. Kuna Mambo nikiandika huwezi kuamini Kama yanafanywa na wadau maarufu unaowajua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…