Aliyoyatamka Nape Nnauye baada ya jaribio la kuuawa Tundu Lissu

Aliyoyatamka Nape Nnauye baada ya jaribio la kuuawa Tundu Lissu

M-mbabe

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2009
Posts
13,203
Reaction score
23,027
Video clip hii inawakilisha silent sympathisers wa Tundu Lissu tuliomo ndani ya CCM. Tupo wengi tu.

Kwenye clip hii Nape Nnauye anaonyesha kuguswa, kusikitishwa na kuwa na hofu kubwa sana baada ya Tundu Lissu kumiminiwa risasi kadhaa. Ni wana CCM wengi tuliguswa na tukio lile ambalo lilituachia bumbuwazi na simanzi kubwa tusijue ni nini kilikuwa kinaendelea nchini.

Miaka 3 baadaye, bado hofu ndani ya chama chetu ni kubwa - ni vile watu tupo kimya tu lakini wengi wamenyamaza kwa ajili ya kutetea vitumbua vyao tu.

Lakini kusema za ukweli, wana CCM ambao hatukuzoea kuyaona na kuyasikia haya yanayoendelea - tunatamani upendo, amani na masikilizano virudi ndani ya chama chetu.

Hivyo basi tunaamini kabisa kwamba kambi ya upinzani ikichukua dola, itatusaidia sana wana CCM kurudi kwenye mstari na kujipanga kwa upya.

Huyu wa kwenye hii clip anatuwakilisha wana CCM wengi tu...

 
Mnataka kumponza mwenzenu tena? Kashaomba msamaha yashaisha sasa mmenza tena, JF bana!!
 
Chadema pambaneni na hali yenu msitafuta public sympathy
 
Nimewaza nikagundua utekaji ulishamiri wakati madelu akiwa waziri mambo ya ndani . ukapungua na kupotea alipotolewa
 
Aliongea kwa kuwa na yeye alionja cha moto. Lakini pia inaonekana anawajua wahusika.
 
Kesi za jinai hazikomi hata Kama muhanga alishasamehe!
Kweli, upo sahihi mkuu!

Na ikipindishwa pindishwa basi vigilantes tutachukua hatua kwa kuwaadhibu wakosaji kadiri ya uzito wa kosa lao!

Mheshimiwa Lissu ameshawasamehe, wapenda haki bado tunataka haki itendeke, huwezi kumpiga mtanzania risasi mchana kweupe tukakuacha hivi hivi ukiendelea kutamba, unastahili kutangulia ukaonane na Mungu akupe adhabu yako mapema
 
Laah! Kiukweli umoja na mshikamano wa nchi vimeharibiwa awamu hii.
 
Back
Top Bottom