Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Ukraine imekubali kupitisha pendekezo la Marekani la kusitisha mapigano mara moja kwa siku 30 katika uvamizi unaoendelea wa Russia dhidi ya nchi hiyo ya Ulaya Mashariki, ikisubiri Moscow ikubali masharti hayo hayo, kulingana na taarifa ya pamoja ya maafisa Jumanne jioni.
"Ukraine ilionyesha utayari wa kukubali pendekezo la Marekani la kutekeleza kusitishwa kwa mapigano kwa muda wa siku 30 mara moja, ambako kunaweza kuongezwa kwa makubaliano ya pande zote, na ambako kunategemea kukubaliwa na kutekelezwa kwa wakati mmoja na Shirikisho la Russia," ilisema taarifa ya pamoja ya Marekani na Ukraine, iliyotolewa baada ya mazungumzo yaliyofanyika Jeddah.
"Maafisa wa pande zote walikubaliana kuteua timu zao za mazungumzo na kuanza mara moja mazungumzo ya kufanikisha amani ya kudumu inayohakikisha usalama wa muda mrefu wa Ukraine."
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, ambaye sasa atawasilisha pendekezo hilo kwa Moscow, aliwaambia waandishi wa habari kuwa "mpira uko uwanjani mwa Warusi" na kwamba iwapo Kremlin haitakubali makubaliano hayo, "basi kwa bahati mbaya tutajua ni nini kinazuia amani."