Tetesi: Alliance Schools yalazimisha watoto kuchanga Tzs100,000 ili kushiriki mahafali 2019/viongozi mlikane hili

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
7,452
Reaction score
3,071
Wanafunzi waliomaliza mitihani yao kidato cha nne Alliance Schools zaidi ya 200, wanatakiwa kuchanga 100,000/-TZS ili kushiriki mahafali ya kidato cha nne 2019. Iwapo kila mwanafunzi atatoa pesa hiyo ni zaidi ya 20,000,000/- Milioni Ishirini,

Mchango huo utahusisha mwanafunzi husika na wazazi wake wawili tu, yaani watu watatu (3).

Ili kuweza kuhusisha wadogo ama wakubwa wa mwanafuzi, yaani watoto wenziwe kwenye famila inabidi kila mtu anayezidi atoke 10,000/-TZS ili kuweza kuingia ndani ya ukumbi wa mahafali, kama huna ni kubaki nje na wanafamilia hawa washindwe kushudia mdogo ama mkubwa wao akitunukiwa cheti.

Yaani imekuwa kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu maana laki moja kwa mahafali ambayo ni wajibu wa shule kwa wahitimu ni changamoto. Watu 3 wakati kiserikali familia ina watu 6. na ni ukweli hapa TZ kuna wajomba shangazi na watoto wao, mara zote kwenye sherehe kama hivi tunashirikishana, iweje bibi au babu kumuona mjukuu wake akihitimu form 4 alazimishwe kulipa TZS 10,000/-? inafahamika kula kwenye mahafali haiwezekani ndugu wote wa wahitimu wakala ama kwa ukweli kuwa itabidi chakula kiwe kingi sana ambacho lazima kitapoteza ubora wake, ama mtu tu hapendi kula nje ya chakula cha familia yake mwenyewe, kwa maana kwenye mahafali kula sio lazima, iweje ulazimishe mtu anayekuja kwenye mahafali ya ndugu yake atoe 10,000 eti lazima ale? unauhakika chakula unachoandaa kinakidhi mahitaji ya kila mshiriki? ya kiafya ya kijamii ya kidini etc?

Tunaomba Viongozi hasa Mkoa maana Rais naye anakazi nyingi na nyinyi ndio wasaidizi wake muingilike kati maana sio haki, kwa vile watoto ni haki yao kufanya na kuhudhuria mahafali isitumike kujipatia pesa kama kitapeli vile maana wazazi wangependa watoto wao washiriki. Ada wazazi walikwisha lipa zote, ni haki ya watoto kufanyiwa mahafali na shule. Hata kama kungekukwa na mchango basi 10,000TZS kwa mtoto. Suala la kula ni la watoto sio wazazi na familia yote maana nyumbani pia watakuwa wameandaa vyakula.

Wazazi na watoto wananyanyasika vile huwezi hitimu alliance ukafanyia mahafali Omega mfano tu.

Kama anaona lazima kuwanyonya wazazi na wahitimu basi agawe vyeti watoto warudi majumbani kwao kula na kunywa, lakni asinyime watoto na ndugu zao haki ya kushiriki mahafali kwa kisingizio cha kuwapa chakula kwa bei ya juu kupita maelezo, chakula ambacho sio lazima wote wanakihitaji na wengine hawataweza kukikutmia kwa sababu za kiafya

Asante kwa msaada wa wenu viongozi serikali-Mwanza
 
Ingekuwa hivyo nadhani ingekuwa shwari sana. Kama bodi ipo lakni, fuatilia mkuu; fuatilia pia kelele zilizokuwepo wakati wa kuchukua watoto kuhusu suala la mahafali kuwa baada ya mitihani tena wiki mbili zaidi hivi yaan tareh Mosi Desemba 2019

Nadhani huo ni muafaka baada ya bodi kupendekeza na wazazi kukubali! Hapo sioni shida!
 
Ingekuwa hivyo nadhani ingekuwa shwari sana. Kama bodi ipo lakni, fuatilia mkuu; fuatilia pia kelele zilizokuwepo wakati wa kuchukua watoto kuhusu suala la mahafali kuwa baada ya mitihani tena wiki mbili zaidi hivi yaan tareh Mosi Desemba 2019
Labda mkuu, sijafuatilia, lakini kwa uzoefu wangu na shule za private jambo kama hili wazazi huwa tunashirikishwa! kama haikuwa hivyo hapo kuna shida!
 
Tunaomba tu Viongozi wa Serikali wafuatilie maana wao wanavyombo macho na mikono mirefu ya serikali, watabaini iwapo ni makubaliano ya wazazi ama ni mtu kutumia uhitaji na haki ya watoto kuwa na mahafali kujipatia pesa
 
Umenena vema, wazazi wanashirikishwa. Sasa tunataka ifuatiliwe uone jinsi wazazi hawakushirikishwa ili iwe wazi kuwa ni haki halali ama la

Labda mkuu, sijafuatilia, lakini kwa uzoefu wangu na shule za private jambo kama hili wazazi huwa tunashirikishwa! kama haikuwa hivyo hapo kuna shida!
na
 
Private sio maana yake iwe holela ama hata kama ni dhulma sawa tu, UTAKUMBUKA WIKI JANA DC Nyamagana aliiingilia kati kanisa moja huko Butimba la ZUmaridi sijui, Kanisa ni imani, wanaokwenda ni wanaoamini na ni hiari, lakni baada ya serikali kusikia kuna ndivyo sivyo pamoja na kuwa watu wanakwenda kwa hiari yao lakn wameingilia. I liked this kind of leadership DC kuingilia iwapo kuna hitirafu hata kama ni hiari ya mtu
 
Mbona michango ya harusi tunatoa na siku hizi Single (kwa maana ya mtu mmoja) inaanzia laki moja (100,000) hatupigi Makelele hivi.

Iweje kwa swala la Mchango (Mahafali) laki moja watu watatu unaanzisha Uzi.

Hebu jaribu kupima hili...
 
Wanafunzi waliomaliza mitihani yao kidato cha nne Alliance Schools zaidi ya 200, wanatakiwa kuchanga 100,000/-TZS ili kushiriki mahafali ya kidato cha nne 2019. Iwapo kila mwanafunzi atatoa pesa hiyo ni zaidi ya 20,000,000/- Milioni Ishirini,

Mchango huo utahusisha mwanafunzi husika na wazazi wake wawili tu, yaani watu watatu (3).

Ili kuweza kuhusisha wadogo ama wakubwa wa mwanafuzi, yaani watoto wenziwe kwenye famila inabidi kila mtu anayezidi atoke 10,000/-TZS ili kuweza kuingia ndani ya ukumbi wa mahafali, kama huna ni kubaki nje na wanafamilia hawa washindwe kushudia mdogo ama mkubwa wao akitunukiwa cheti.

Yaani imekuwa kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu maana laki moja kwa mahafali ambayo ni wajibu wa shule kwa wahitimu ni changamoto. Watu 3 wakati kiserikali familia ina watu 6. na ni ukweli hapa TZ kuna wajomba shangazi na watoto wao, mara zote kwenye sherehe kama hivi tunashirikishana, iweje bibi au babu kumuona mjukuu wake akihitimu form 4 alazimishwe kulipa TZS 10,000/-? inafahamika kula kwenye mahafali haiwezekani ndugu wote wa wahitimu wakala ama kwa ukweli kuwa itabidi chakula kiwe kingi sana ambacho lazima kitapoteza ubora wake, ama mtu tu hapendi kula nje ya chakula cha familia yake mwenyewe, kwa maana kwenye mahafali kula sio lazima, iweje ulazimishe mtu anayekuja kwenye mahafali ya ndugu yake atoe 10,000 eti lazima ale? unauhakika chakula unachoandaa kinakidhi mahitaji ya kila mshiriki? ya kiafya ya kijamii ya kidini etc?

Tunaomba Viongozi hasa Mkoa maana Rais naye anakazi nyingi na nyinyi ndio wasaidizi wake muingilike kati maana sio haki, kwa vile watoto ni haki yao kufanya na kuhudhuria mahafali isitumike kujipatia pesa kama kitapeli vile maana wazazi wangependa watoto wao washiriki. Ada wazazi walikwisha lipa zote, ni haki ya watoto kufanyiwa mahafali na shule. Hata kama kungekukwa na mchango basi 10,000TZS kwa mtoto. Suala la kula ni la watoto sio wazazi na familia yote maana nyumbani pia watakuwa wameandaa vyakula.

Wazazi na watoto wananyanyasika vile huwezi hitimu alliance ukafanyia mahafali Omega mfano tu.

Kama anaona lazima kuwanyonya wazazi na wahitimu basi agawe vyeti watoto warudi majumbani kwao kula na kunywa, lakni asinyime watoto na ndugu zao haki ya kushiriki mahafali kwa kisingizio cha kuwapa chakula kwa bei ya juu kupita maelezo, chakula ambacho sio lazima wote wanakihitaji na wengine hawataweza kukikutmia kwa sababu za kiafya

Asante kwa msaada wa wenu viongozi serikali-Mwanza
Hizi nazo ni tabia za kudandia treni kwa mbele; kama humudu malipo ya hizo shule si shule za bure zipo?
 
Acha kupotosha ww mtoa mada. Wazazi tuliridhia kutoa hicho kiwango kwa sababu kadhaa ikiwemo kupanda bei ya bidhaa, muziki, mapambo ya ukumbi, vyakula n.k.

Na tulisema mahafali ya mwaka huu yawe tofauti na miaka mingne na ww ulikubali. Sasa vip unakuja huku tena kulalama?
 
Mzazi maskini usipeleke shule za Wenye pesa wakati wewe maskini koma kabisa

Nilishawahi kufanya kaxi shule moja ya private ya wahindi ambapo na watoto waswahili husoma.Ada kwa mwaka Ni Kama milioni Saba .Wakasema kila Mzazi anatakiwa kuchangia milioni tano kwa ajiri ya kutengeneza maabara ya kisasa ya komputa .Mzazi mmoja akanyoosha mkono akasema hayo mbo Ni ya wamiliki wa shule yeye Kama mzazi hayamhusu akatishia kumtoa mwanae .Akaxomewa na wazazi waliobaki mpaka mwenyekiti akawabia wamsamehe .Kwa hasira alimtoa mwanae kwenye ile shule.

Somesha shule za kipato Cha saizi yako usiige kunya kwa tembo

Laki mbili unaona nyingi shule Kama hiyo.Nenda kadomeshe za serikali Ni bure
 
Graduation sio lazima mi mzee wangu alisemaga atakuja kwenye graduation yangu ya degree na kweli alikaza sasa graduation ya form four si upuuzi tu watu graduation za degree hawahudhurii sembuse hii ya form four sijui form six. Mzee kama huna hela kausha hautakufa kukosa iyo graduation
 
Yaani mimi kusema ukweli nilijiuliza sana umuhimu wa wazazi kwenda kwenye graduation. Mimi O level,A level yaani hakuna ndugu yangu alokuja kwenye graduation. Na niliona poa tu. University ndo kabisa hata kwenye graduation sikwenda maana nilikuwa kazini tayari. Yaani mimi sherehe wala huwa sioni kabisa umuhimu wake.
 
Back
Top Bottom