Wanafunzi waliomaliza mitihani yao kidato cha nne Alliance Schools zaidi ya 200, wanatakiwa kuchanga 100,000/-TZS ili kushiriki mahafali ya kidato cha nne 2019. Iwapo kila mwanafunzi atatoa pesa hiyo ni zaidi ya 20,000,000/- Milioni Ishirini,
Mchango huo utahusisha mwanafunzi husika na wazazi wake wawili tu, yaani watu watatu (3).
Ili kuweza kuhusisha wadogo ama wakubwa wa mwanafuzi, yaani watoto wenziwe kwenye famila inabidi kila mtu anayezidi atoke 10,000/-TZS ili kuweza kuingia ndani ya ukumbi wa mahafali, kama huna ni kubaki nje na wanafamilia hawa washindwe kushudia mdogo ama mkubwa wao akitunukiwa cheti.
Yaani imekuwa kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu maana laki moja kwa mahafali ambayo ni wajibu wa shule kwa wahitimu ni changamoto. Watu 3 wakati kiserikali familia ina watu 6. na ni ukweli hapa TZ kuna wajomba shangazi na watoto wao, mara zote kwenye sherehe kama hivi tunashirikishana, iweje bibi au babu kumuona mjukuu wake akihitimu form 4 alazimishwe kulipa TZS 10,000/-? inafahamika kula kwenye mahafali haiwezekani ndugu wote wa wahitimu wakala ama kwa ukweli kuwa itabidi chakula kiwe kingi sana ambacho lazima kitapoteza ubora wake, ama mtu tu hapendi kula nje ya chakula cha familia yake mwenyewe, kwa maana kwenye mahafali kula sio lazima, iweje ulazimishe mtu anayekuja kwenye mahafali ya ndugu yake atoe 10,000 eti lazima ale? unauhakika chakula unachoandaa kinakidhi mahitaji ya kila mshiriki? ya kiafya ya kijamii ya kidini etc?
Tunaomba Viongozi hasa Mkoa maana Rais naye anakazi nyingi na nyinyi ndio wasaidizi wake muingilike kati maana sio haki, kwa vile watoto ni haki yao kufanya na kuhudhuria mahafali isitumike kujipatia pesa kama kitapeli vile maana wazazi wangependa watoto wao washiriki. Ada wazazi walikwisha lipa zote, ni haki ya watoto kufanyiwa mahafali na shule. Hata kama kungekukwa na mchango basi 10,000TZS kwa mtoto. Suala la kula ni la watoto sio wazazi na familia yote maana nyumbani pia watakuwa wameandaa vyakula.
Wazazi na watoto wananyanyasika vile huwezi hitimu alliance ukafanyia mahafali Omega mfano tu.
Kama anaona lazima kuwanyonya wazazi na wahitimu basi agawe vyeti watoto warudi majumbani kwao kula na kunywa, lakni asinyime watoto na ndugu zao haki ya kushiriki mahafali kwa kisingizio cha kuwapa chakula kwa bei ya juu kupita maelezo, chakula ambacho sio lazima wote wanakihitaji na wengine hawataweza kukikutmia kwa sababu za kiafya
Asante kwa msaada wa wenu viongozi serikali-Mwanza