Uchaguzi 2020 Ally Bananga atia nia ubunge Arusha mjini - CHADEMA

Kati ya marafiki zake na mke wake ambae alikuwa mbunge viti maalum CDM,na ambae ametia nia kugombea ubunge Tabora mjini nani yupo karibu nae?. Kwa nini awafate rafiki zake nasio aambatane na mkewe kukipigania chama?.
 

Bila kupinga maelezo yako yote mazuri. Ila tujikite hapo kuwa anaweza kushirikina na wanachama, wananchi na serikali. Kwa Arusha ninayoijua mimi ni kuwa imeshavuka hatua ya maendeleo ya kuisujudia serikali, maana miundombinu mbinu yote ipo, kama shule gov+private, hospital gov+private, barabara, umeme, maji nk. Sioni chochote ambacho mbunge yoyote anapaswa kujinyenyekeza kwenye siasa za kusujudia serikali, bali kushirikiana na serikali kwa mujibu wa serikali kutekeleza wajibu kama mkusanya kodi. Labda kama maelezo yako mazuri, yamejikita kwenye tofauti zako binafsi na Lema.
 
Itategemea siku hiyo wameamkaje
 
Kati ya marafiki zake na mke wake ambae alikuwa mbunge viti maalum CDM,na ambae ametia nia kugombea ubunge Tabora mjini nani yupo karibu nae?. Kwa nini awafate rafiki zake nasio aambatane na mkewe kukipigania chama?.
Mbona Kafulila alimuacha mke wake yeye akaenda kuunga juhudi? Lakini vilevile kwa mfano huo huo Jesca alikataa kumfuata mume wake upande wa pili na ameendelea kukipigania chama chake kwa nguvu zake zote. Kwa huyu bwana lolote linawezekana. Tofauti yake na Lema ni kuwa Lema ameonyesha kwa vitendo kuwa yeye ni mfia chama, huyu bwana bado. Atatakiwa afanye hivyo maana hili swali halikwepeki. Uzuri wake ni kuwa hakuungana na rafiki zake na kuna uwezekano mkubwa kuwa nae ni mfia chama. Ila ni lazima ajue kuwa hawezi kuwa na urafiki wa karibu na wapinzani wa chama chake katika wakati huu wa uchaguzi.

Amandla...
 

Kafulila alimfuata nani ccm?, aliwafata rafiki zake?..

Suala sio kumfuata mtu suala niuamuzi wako binafsi, Kama akiamua kukaa atakaa na akiamua kuondoka ataondoka. Mimi nachosema hapa nikuwa wapitishwe kwenye Kura za maoni atakaeshinda ndio awe mgombea haya yakusema fualani anatumika fulani hivi huo niupuuzi.

Slaa alizunguka nchi kusema Zitto anatumika na ccm, leo wote tunafaham Slaa yuko wapi na Zitto yuko wapi. Lijuakali kakaa keko/Segerea miezi lakini haikuwa kigezo Cha kutounga juhudi.

Kwahio kukaa gerezan sio kipimo pekee cha kusema kuwa hawezi unga juhudi Jambo lamsingi tuache demokrasia ichukue mkondo wake .Na atakaeshindwa akubali kushirikiana na mwenzake ili jimbo liendelee kubaki CDM.
 
Mkuuu nakuunga mkono kwa asilimia ukishachukua mara kumi achia damu changa katagute jimbo korofi ugombee maana tayari umaarufu na pesa unazo
 
Mkuuu nakuunga mkono kwa asilimia ukishachukua mara kumi achia damu changa katagute jimbo korofi ugombee maana tayari umaarufu na pesa unazo
Ndio ukomavu wenyewe ..
 
Regardless Slaa nae ni Ccm kwa sasa lkn haiondoi ukweli Zitto alikua anatumika na CCM kuivuruga Chadema.
 
Mimi Kafulila simjui kiasi cha kusema kuwa hakuwa na marafiki CCM ambao walisaidia kumshawishi ahamie huko. Vile vile simjui Banaga kiasi cha kusema kwa uhakika kuwa anatumika. Bahati mbaya uliishia kusoma nilichoandika kuhusu Kafulila. Hukusoma niliposema kuwa mke wake Kafulila hakumfuata mumewe CCM na amethibitisha pasipo shaka kuwa ni mfia chama chake. Banaga nae anaweza kuwa ni mfia chama kama alivyo mke wake Kafulila. Na inawezekana kabisa Lema kuwafuata nyendo za wakina Lijualikali na Slaa ingawa kwa mtazamo wa wengi huo uwezekano ni mdogo. Ninachokisema ni kuwa maswali ya commitment kwa chama chake yataulizwa zaidi kwa Banaga kuliko kwa Lema. Lakini commitment hiyo itathibitishwa zaidi kwa kila mmoja jinsi watakavyopokea kutoteuliwa nao. Kama watakubali matokeo na kumpigania atakaeteuliwa itakuwa ni uthibitisho zaidi kuwa wao ni wanachama committed wa chama chao. Kama watasusa au watahamia chama kingine basi itakuwa wamethibitisha kuwa hawakuwa committed.

Amandla...
 
Regardless Slaa nae ni Ccm kwa sasa lkn haiondoi ukweli Zitto alikua anatumika na CCM kuivuruga Chadema.
Jambo lamsingi hakuna mfia chama, Jambo lakuelewa nimuda ukifika hakuna wakuzuia. Kwahiyo kumuhukumu Banaga eti kisa rafiki ake ni Msando sio kumtendea haki. Hakuna aliekua mfia chama CDM Kama Slaa nahata Mbowe mwenyewe hakua mfia chama kama alivyokuwa Slaa lakini tunajua leo kila mtu kasimama upande upi.Jambo lamsingi Kura za maoni zitaamua .
 
Leta ushahidi wa Dr Slaa kuchukua kadi ya CCM.
Kumbe huwa hamufuatilii mambo?? Dr slaa aliwahi hojiwa ITV miaka hiyo tena akiwa Katibu mkuu wa chadema kuhusu kumiliki kadi ya ccm, alijibu hv, kadi ni mali ya mwanachama hvyo kadi ni mali yng na ni kumbukumbu yangu...hvyo anayo ya ccm na pia anayo ya chadema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…