RUSTEM PASHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2016
- 4,707
- 11,365
Pia atakaepigiwa Kura za maoni nakushinda ,huko juu wasije wakakata majina ya watu, watakuwa hawana tofauti nayule aliesema itategemea nimeamkaje.Mimi Kafulila simjui kiasi cha kusema kuwa hakuwa na marafiki CCM ambao walisaidia kumshawishi ahamie huko. Vile vile simjui Banaga kiasi cha kusema kwa uhakika kuwa anatumika. Bahati mbaya uliishia kusoma nilichoandika kuhusu Kafulila. Hukusoma niliposema kuwa mke wake Kafulila hakumfuata mumewe CCM na amethibitisha pasipo shaka kuwa ni mfia chama chake. Banaga nae anaweza kuwa ni mfia chama kama alivyo mke wake Kafulila. Na inawezekana kabisa Lema kuwafuata nyendo za wakina Lijualikali na Slaa ingawa kwa mtazamo wa wengi huo uwezekano ni mdogo. Ninachokisema ni kuwa maswali ya commitment kwa chama chake yataulizwa zaidi kwa Banaga kuliko kwa Lema. Lakini commitment hiyo itathibitishwa zaidi kwa kila mmoja jinsi watakavyopokea kutoteuliwa nao. Kama watakubali matokeo na kumpigania atakaeteuliwa itakuwa ni uthibitisho zaidi kuwa wao ni wanachama committed wa chama chao. Kama watasusa au watahamia chama kingine basi itakuwa wamethibitisha kuwa hawakuwa committed.
Amandla...