Ally Bananga: Nikifika mbinguni (peponi) nikikuta Mama Samia hayupo natoka peponi

Ally Bananga: Nikifika mbinguni (peponi) nikikuta Mama Samia hayupo natoka peponi

Ni mhuni mmoja tu wa hapo Mbauda hana jipya mke wake ni mmoja wa wale covid 19 walipo mle bungeni kinyume cha sheria.

Huwa anaburuzwa sana na mkewe baada ya kukosa ulaji (alichukua form kugombea ubunge Arusha kupitia CDM ila Lema ndie aliepitishwa) na hana mishe yoyote zaidi ya kulewa bar asubuhi mpaka usiku.

Binafsi namfahamu vizuri tu maana nimezaliwa na kukulia mtaa moja na yeye.
Hahahahahahah njaa kali aisee! Mke kukulisha miaka 5 lazma akuburuze vibaya mno!
 
Hata kama ni kujipendekeza lakini sio kwa maneno haya!

Angesifia yote mazuri aliyofanya. Mfano 1.5T ilivyogawanywa kwenye maendeleo, uhuru wa vyombo vya habari, Kukemea TRA kutokutumia nguvu kwenye ukusanyaji wa kodi na n.k

Haya mambo ya peponi hata huyo unayemsifia anaweza kuona huyu ni wale “handle with care”!!
Heheheheh atakapopewa shavu muendelee kumsakama hivyo hivyo wakati anakula per diem zake 😀
 
. M
Mtume S.a.w alitutahadharisha sana kupenda (kujipendekeza) kupitiliza kwa kuwa utajikuta unakufuru tu!

Huyu Mtoto anadhan issue ya Kuingia Peponi ni kama kuingia Bungeni tu

Swahaba Mkubwa sana wa Bw. Mtume s.a.w ambae alikuwa Mweusi (Bilal bin Rabbah) alisema hata akiwa kishaingiza Mguu mmoja ndani ya Pepo bado hatokuwa na uhakika wa kuingia Peponi lakin anatokea mtu kwa kujipendekeza tu anakufuru kwa kumpa Mungu Masharti eti akitaka kumuingiza Peponi lazima na fulani nae aingie…

vyeo vya Kidunia vinaishia huku huku huko hakutakuwa na mambo ya 'kupita bila ya kupingwa'
Mkuu weka ushahidi hata sura ama mahadith alipotahadharisha
 
Kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu!! Kwenye siasa ni mwendo wa unafiki na kujitoa ufahamu kwa kwenda mbele!! Kwenye siasa utafikiri wamelogwa!! Kiongozi mkuu utakuta anajua kabisa kuwa sifa wanazompa hana na ni unafiki tu wa kujipendekeza kwa maslahi binafsi lakini bado utakuta kiongozi huyo anazifurahia sifa hizo huku akijua kabisa ni za unafiki na sifa hizo hana!! Siwezi kushangaa maneno kama hayo kusemwa na Tundu Lisu siku moja!! Nani aliyekuwa anaaminika kama Dr Slaa?? Leo yuko wapi?? Maana ya siasa ni SI HASA!!
 
Wanasiasa walivyo wa ovyo, unaweza kukuta alikuwa anamaanisha kinyume chake!! Yaani akifika jehanamu halafu asimkute atashangaa sana!! Maana kwa unafiki huo jehanamu ndiyo ana uhakika wa kufika!!
 
Kumbuka ameongea kisiasa na si kwenye hadhar ya mahubiri,hata yeye na aliyekua akiwahutubia wote wanajua yeye hajui kesho,na huko peponi hakuna anayejua kweli kama kupo,hata wewe hujui na hautajua

Kwa hivyo huna sababu ya kuanzisha mada dhidi ya kauli za huyo sijui Bananga umesema mi simjui,nimemuona jana

Shutuma zake juu ya kauli yake binafsi ningeiona ina ukakasi iwapo angezungumzia kwenye mkutano wa dini,sema waTanzania kila kitu hua mnajadili tu
Kwa hiyo ukiongea kisiasa ndio unaongea ujinga kama huu...hiyo definition ya siasa ndio hii....very stupid indeed
 
Anasema hivyo kwa sababu anajua hilo haliwezekani
 
Kwa kaliba yake Bananga anatarajia kupata uteuzi gani? Huyo anafaa kuwa mwanaharakati tu au Diwani apambane kwenye vikao huko.
 
katika kuongea kuna ile kupitiliza.huenda kwa furaha aliyoipata ya kuongea mbele ya amir jesh mkuu akaona atie na kibwagizo hicho.ingawa kimekaa sio vizur kwa mtu wa din hasa hasa muslim,huwez kukata kaul flan atakua pepon flan moton kule nimpazito panataka khofu, labda anaweza kuingia katika mlango wa dharura wa furaha iliuopitilza ndio akasema hayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbuka ameongea kisiasa na si kwenye hadhar ya mahubiri,hata yeye na aliyekua akiwahutubia wote wanajua yeye hajui kesho,na huko peponi hakuna anayejua kweli kama kupo,hata wewe hujui na hautajua

Kwa hivyo huna sababu ya kuanzisha mada dhidi ya kauli za huyo sijui Bananga umesema mi simjui,nimemuona jana

Shutuma zake juu ya kauli yake binafsi ningeiona ina ukakasi iwapo angezungumzia kwenye mkutano wa dini,sema waTanzania kila kitu hua mnajadili tu

Kwa hiyo wewe bwege mtu ana kufuru kwa kufanya au kutamka hiyo kufuru akiwa eneo la ibada?
Wewe ndio bwege kabisa
Mfano Mimi nikae zangu barabarani nianze kutoa maneno ya kashfa Juu ya Mungu kwa kuwa tu sipo Kwenye eneo la mahubiri utakuwa sawa
 
Kunausemi unasemaga ukistaajabu ya Musa...

Leo katika jiji la Arusha aliyekuwa kamanda wa chama cha Demcrasia na Maendeleo Chadema Ally Bananga alirudisha kadi ya chama hicho katika mkutana mkubwa wa adhala wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Hassan, Kamanda huyo wa zamani ametoa kauli ya ajabu na kushanga.

Pamoja na kuonge vizuri katika hotuba yake kisiasa lakini ametoa kauli ya ajabu sana hasa kwetu sisi viongozi wa dini imetupa ukakasi mkubwa sana kwa ndugu huyo. Bananga amesema kuwa kama akifika mbinguni na kukuta mama Samia hayupo huko peponi atatoka huko peponi yeye. Sijui atatoka kumtafuta wapi.

Kauli hii nzito na yakushangazana ya kipagani na ya fedhea kwa Mungu wetu imeleta gumzo katika makundi yetu mengi ya wasapu ya viongozi wa dini wakiwemo wachungaji, mashekh, maaskofu, mitume na manabii. Katika haya magrupu viongozi wengi wamebaki midomo wazi na wengine kutatoa macho kanakwamba wanatengeneza saa kwa kukosa pakuanzia kujadili.

Kwa msikilizaji wa kufikiri na akili aliyekuwa anamsikiliza Bananga katika hotuba yake alikuwa kama au likuwa anafanya intavyuu ya kuomba kazi kwa Mhs. Rais na si vinginevyo. Katika maongezi yake alionyesha uzoefu wake wa kazi kuwa anaweza na amekaa katika uongozi kwa vipindi kadhaa na amefanya kadha wa kadha ikiwemo uwazishwaji wa jambo fulani. Alizidi kwenda mbali kwa kusema anauwezo wa kufanya mambo magumu na mchapakazi hivyo anaomba asiachwe benchi atumike katika serikali.

Bananga ambaye mara nyingi amekuwa akitishia kurudisha kadi hiyo ya Chadema lakini leo ametumia mwanya huo kama fulsa kurudisha kadi hiyo na kuomba kazi kwani amekuwa benchi kwa muda sasa kisiasa ukilinganisha na mkewe kuwa mbunge wa viti maarumu kupitia Chadema.

Bananga ambaye Mungu amempa neema ya kutembelea upepo kwani zamani alikuwa mwanachama mtiifu wa CCM na baada ya kuona chama hicho ilikuwa ikidorola mika ya 2013 alibadili gia na kuhamia Chadema, lakini leo kilichotokea CCM kinatokea Chadema hivyo anabadili tena gia na kurudi CCM kusaka fulsa kama alivyosikika katika hotuba yake ya kuombakazi.

Mimi kama mtumishi wa Mungu namshauri Bananga kuomba kitubio kwa Mwenyezi Mungu kwa kauli yake ya kibuli cha uzima, kauli yake ni chukizo kwa Mungu kwani haikubaliki kanisa, haikubaliki msikitini na haikubaliki hata kindagateni mpaka chuo kikuu.
Peponi sio na ukumbi wa Cinema
 
Nawashauri vijana ingieni siasa baada ya kuwa na kazi za uhakika, siasa ifanye kama wito na si ajira rasmi, haya ndiyo matokeo yake kila siku kijana na furushi mgongoni kuhama hama kisa uchumi mfukono umeyumba.
 
Back
Top Bottom