Ally Bananga: Nina kiapo na mke wangu, nitamlinda kwa gharama ya damu yangu

Ally Bananga: Nina kiapo na mke wangu, nitamlinda kwa gharama ya damu yangu

Ukijua ma boss wako wanaimba usafi huku wanaogelea kwenye uchafu unakua smart sana

Ally Bananga ni mwanachadema mwenye akili kubwa sana zaidi ya watu wanavyomwangalia

Kwangu alikua diwani bora kwa kipindi chote cha uwakilishi wake na niliwahi kuongea hapa kabla hata mkewe hajawa mbunge
Uchafu upi aliouona na kuusemea?

Nadhani tunatofautiana kwenye tafsiri ya neno smart. Mimi mtu anaesema kuwa mke wake ni zaidi ya katiba hana u smart wowote. Ni kama yule aliyesema human rights hazina maana yeyote.

Samahani lakini huyu jamaa anaonekana ni opportunist tu. Hapo anataka kupandisha dau tu.

Amandla...
 
Ukijua ma boss wako wanaimba usafi huku wanaogelea kwenye uchafu unakua smart sana

Ally Bananga ni mwanachadema mwenye akili kubwa sana zaidi ya watu wanavyomwangalia

Kwangu alikua diwani bora kwa kipindi chote cha uwakilishi wake
Wezi wua kura wakafanya yao[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Sio sababu ya mkewe kuwa mbunge, Bananga ni akili kubwa.... anajua kuishi ndani ya itikadi bila kuathiri jamii
Bananga hanaga akili za kushikiliwa
 
"Mimi ni mwanachama wa CHADEMA, Suala la wabunge 19 wa viti maalumu ambao Chama chetu kinasema hakiwatambui, mke wangu (Hawa Bananga) pia ni miongoni mwao na katika vitu ambavyo nimekuwa nikijiepusha kuvizungumza ni suala hili kwasababu bado maamuzi yako ndani ya chama, kuliweka hili kwa ufupi mimi nitasimama aliposimama mke wangu kwasababu sikufunga naye ndoa CHADEMA, sikufunga naye ndoa mitandaoni nilifunga naye ndoa msikitini, kiapo changu kwake ni kumlinda kwa gharama ya damu yangu....lolote lenye udhaifu kwake ni wajibu wangu kulipa uimara, ndio kitu cha thamani ninachomiliki, nitamlinda mama wa watoto wangu "-Mwanasiasa Ally Bananga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Nimemsikiliza Star Tv hakika hatuna mwanachama pale ,Kashaenda CCM yule ni matter of time.
 
Uchafu upi aliouona na kuusemea?

Nadhani tunatofautiana kwenye tafsiri ya neno smart. Mimi mtu anaesema kuwa mke wake ni zaidi ya katiba hana u smart wowote. Ni kama yule aliyesema human rights hazina maana yeyote.

Samahani lakini huyu jamaa anaonekana ni opportunist tu. Hapo anataka kupandisha dau tu.

Amandla...
Uchafu huko upo mwingi
Ila ule wa kumsafisha waliyemwita fisadi papa lowasa ili wamle pesa ulitia fora
 
Mtu akielekea kuhamia kwenu au akitofautiana na chama chake ndio mnagundua kuwa siku alikuwa na akili sana!

Sasa huyu genius wako anasema anamsupport mke wake kwa sababu alimuoa msikitini na sio kwa sababu yuko sahihi! Heri angesemq kuwa mpango wote walisuka pamoja. Kazi kweli ipo.

Amandla...
Kama kumbukumbu zangu ziko vizuri; bananga, lema na mawazo walikuwa TLP kabla ya kuhamia chadema.
 
Kuna point kaongea ya muhimu.Kuwa si kila Jambo viongozi wa Chadema wanapaswa kuhangaika nalo.Mambo madogomadogo kama haya ya akina Diamond yanawapotezea focus na muda CHADEMA.
Ila kuna sehemu sijamuelewa,aliposema yupo tayari kurudisha kadi kwa ajili ya familia.Amemaanisha kuwa endapo rufaa waliyokata wale 19 endapo watashindwa na kufukuzwa kabisa naye atahama chama?
 
Huo ni ulafi sasa
 
Hili suala la Diamond sio la Chadema. Lissu amesema wazi kuwa ni msimamo wake binafsi. Ingawa inawezekana wengi walio nyuma ya hiyo kampeni wana mapenzi na Chadema haina maana kuwa Chadema kama chama kinawaunga mkono.

Hiyo ya kurudisha kadi ni bora angeirudisha tu na ahamie upande ambako ataweza kumpokea vizuri mke wake kama rufaa yake itashindwa. Kuoana na mtu hakumaanishi kuwa mtakubaliana kila kitu. Cha msingi ni kuheshimiana katika kutofautiana kwenu. Kuna familia nyingi tu ambazo wanandoa wana imani lakini maisha yanaendelea vizuri tu. Kuna nyingi tu ambamo wanandoa ni mashabiki wa timu tofauti za mpira lakini ndoa zao zinabaki imara. Hivyo hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa kwenye siasa. Muunge mkono mke kwa sababu yuko sahihi na sio kwa sababu ni mke wako. Sidhani kama kuna mtu Chadema mwenye mpango wa kumdhuru mke wake hadi afikie kusema atamlinda kwa damu yake yote. Kwa maneno haya amekuwa sawa na wakina Lijualikali kwa kuona kuwa hawezi kupata bila ku insinuate kuwa uongozi wa Chadema ni majambazi na wanaweza kumdhuru mtu waliotofautiana nao. Hajafanya vizuri.

Amandla...
 
Back
Top Bottom