Ally Bananga: Nina kiapo na mke wangu, nitamlinda kwa gharama ya damu yangu

Ally Bananga: Nina kiapo na mke wangu, nitamlinda kwa gharama ya damu yangu

Nimemsikia Ally Bananga kwenye mahojiano, nadhani amepanic nakuanza vita bila kujua anapambana na nani. Amepambana na Lissu, Lema, Mnyika kwa maana wamekosea sehemu fulani kutokana na tweet zao juu ya kukutana na Rais, Diamond pamoja na wabunge 19.

Anapohojiwa msimamo wake kuhusu wabunge 19 anaeleza kwamba familia Kwanza Katiba baadaye. Najiuliza anaamini hiki ndicho wananchi wanachokihitaji? Leo viongozi wote wa upinzani wakiwaza familia zao watapata muda wakuwaza Katiba mpya?

Anasema wakutane na shibuda Kwanza kabla ya kwenda kuonana na Rais Kama takwa lakukukuna linavyotaka, je leo tunaamini shibuda anakubaliana na agenda za Chadema wanazotaka kuziwasilisha kwa Rais? Je waende kukutana na Rais kama fasheni au waende kwa msingi wa mahitaji ya hoja zao.

Anadai atamuunga mkono Diamond, lakini wengine wanaopingana na Diamond anadai wamekosa agenda. Kwanini anaamini kwake kumsapoti diamond ni agenda lakini wengine mmojammoja awapaswi kumpinga diamond? Ni wapi chama kimetoa msimamo wake juu ya bet ya Diamond?

Lakini pia overconfidence inamwondoa kwenye mjadala nakufikia kuona Kama alistahili kuwa mgombea wa Chadema Arusha na si Lema. Je Kama alikuwa na kinyongo juu ya lema kwanini asimwambie?
Uzoefu unaonyesha ukianza kuona kiongozi wa cdm anaoongea lugha kama hizo za Bananga ujue yuko njiani kurejea ccm.
 
Kwahiyo hata kama mkewe akitoa ngono na kuwa mwizi anasimama naye? Jinga kubwa
 
"Mimi ni mwanachama wa CHADEMA, Suala la wabunge 19 wa viti maalumu ambao Chama chetu kinasema hakiwatambui, mke wangu (Hawa Bananga) pia ni miongoni mwao na katika vitu ambavyo nimekuwa nikijiepusha kuvizungumza ni suala hili kwasababu bado maamuzi yako ndani ya chama.

Kuliweka hili kwa ufupi mimi nitasimama aliposimama mke wangu kwasababu sikufunga naye ndoa CHADEMA, sikufunga naye ndoa mitandaoni nilifunga naye ndoa msikitini, kiapo changu kwake ni kumlinda kwa gharama ya damu yangu.

Lolote lenye udhaifu kwake ni wajibu wangu kulipa uimara, ndio kitu cha thamani ninachomiliki, nitamlinda mama wa watoto wangu

"-Mwanasiasa Ally Bananga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Chanzo: Star TV
Ndugu yangu Bananga, hatuzungumzii mke wa mtu hapa. Tuelewane hapo. Tunachozungumzia ni uhalali wa wanawake 19 wa CHADEMA kuwepo Bungeni visivyoeleweka. Sidhani hata wewe unaweza kutueleza vizuri tukakuelewa. Wabunge wote wametokana na vyama mbalimbali vya Siasa. Hawa hawakufuata taratibu za chama kuingia Bungeni. Hata mimi nafurahi wawepo Bungeni, tena wasemaji wazuri tu. Lakini uhalali wao ukoje Bananga.
 
Uchafu upi aliouona na kuusemea?

Nadhani tunatofautiana kwenye tafsiri ya neno smart. Mimi mtu anaesema kuwa mke wake ni zaidi ya katiba hana u smart wowote. Ni kama yule aliyesema human rights hazina maana yeyote.

Samahani lakini huyu jamaa anaonekana ni opportunist tu. Hapo anataka kupandisha dau tu.

Amandla...
Umesema vema: HAKUNA ALIYE ZAIDI YA KATIBA, hususan ya nchi yake
 
Siyo mdogo kwenye siasa hasirani kama unamaanisha miaka aliyoanza kujishughulisha na siasa. Labda kama ungesema udogo kwa maana ya uimara wake kisiasa( Political and ideological stand). Mimi namuona mdogo Kwa maana ya mtizamo wake( ideological perspective)

Mke wake ni moja ya watu walio bungeni kimakosa, na kwa sababu ni familia yake, kama alikuwa hana ubavu wa kusema shida ya mkewe hadharani, angenyamaza badala ya kuja public na kusema atamlinda Kwa Damu.

Labda nimfahamishe Bananga kwamba uzuri wa mtu yeyote, ni pale anapoweza kusimamia ukweli hata kwa gharama ya kifo. ( The highest good of any individual is to die for the truth).

Na kwa maana yake, hata Kwa gharama ya kuachwa na mkewe. Kama huwezi Hilo " hutufai na hafai kufanya siasa zenye substances,labda kama ni siasa za kuganga njaa.
Jamani tuheshimu Wanawake, wametuzaa. Napendekeza mjadala wa Mrs Bananga ufungwe. Nina mashoka 5 hapa makamanda 5 waje upenu niwagee waende kukata tamaa,
 
Good, good! Mwisho wa siku lazima mtu asimame kwenye ukweli. Familia kwanza kabla ya kitu chochote. Huwezi kutelekeza famila halafu eti ukawa mtiifu wa chama. Hata Lissu na Lema walikimbilia nje ya nchi na familia zao! Hawakukimbia na Chadema wala wana Chadema!
Mkuu umeandiki nini!! Huna elezea hoja ya ku-support mada. Kwa ujumla mtoa mada ameshindwa kabisa kutetea au kujenga hoja yake. Je huyo mkeo ukimkuta chocho hutamuhoji anatafufuta nini huko chocho? Je unajua vitabu vyote vya DINI vinatambua neno TALAKA, kwa nini neno hilo Lipo? TAFAKALI SANA.
 
Kuna point kaongea ya muhimu.Kuwa si kila Jambo viongozi wa Chadema wanapaswa kuhangaika nalo.Mambo madogomadogo kama haya ya akina Diamond yanawapotezea focus na muda CHADEMA.
Ila kuna sehemu sijamuelewa,aliposema yupo tayari kurudisha kadi kwa ajili ya familia.Amemaanisha kuwa endapo rufaa waliyokata wale 19 endapo watashindwa na kufukuzwa kabisa naye atahama chama?
Ndio maana yake. Kwa maana nyepesi ni kuwa, yupo CHADEMA kwa ajili ya UJIRA wa AJIRA ya mke wake na pindi AJIRA ikisitishwa naye anasitisha uwanachama wa chama chake.
 
"Mimi ni mwanachama wa CHADEMA, Suala la wabunge 19 wa viti maalumu ambao Chama chetu kinasema hakiwatambui, mke wangu (Hawa Bananga) pia ni miongoni mwao na katika vitu ambavyo nimekuwa nikijiepusha kuvizungumza ni suala hili kwasababu bado maamuzi yako ndani ya chama,

Kuliweka hili kwa ufupi mimi nitasimama aliposimama mke wangu kwasababu sikufunga naye ndoa CHADEMA, sikufunga naye ndoa mitandaoni nilifunga naye ndoa msikitini, kiapo changu kwake ni kumlinda kwa gharama ya damu yangu....

Lolote lenye udhaifu kwake ni wajibu wangu kulipa uimara, ndio kitu cha thamani ninachomiliki, nitamlinda mama wa watoto wangu

"-Mwanasiasa Ally Bananga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Chanzo: Star TV
Huu ndio uanaume
 
Chadema hawatambui uchaguzi wa 2020 hawachukui ruzuku wabunge wale 19 chadema haiwatambui washawafuza uanachama najiuliza wanaendelea kuwashupalia ili kiwe nini wakivuliwa ubunge je chadema watapeleka wabunge wengine au inakuaje apo?
 
Nimemsikia Ally Bananga kwenye mahojiano, nadhani amepanic nakuanza vita bila kujua anapambana na nani. Amepambana na Lissu, Lema, Mnyika kwa maana wamekosea sehemu fulani kutokana na tweet zao juu ya kukutana na Rais, Diamond pamoja na wabunge 19.

Anapohojiwa msimamo wake kuhusu wabunge 19 anaeleza kwamba familia Kwanza Katiba baadaye. Najiuliza anaamini hiki ndicho wananchi wanachokihitaji? Leo viongozi wote wa upinzani wakiwaza familia zao watapata muda wakuwaza Katiba mpya?

Anasema wakutane na shibuda Kwanza kabla ya kwenda kuonana na Rais Kama takwa lakukukuna linavyotaka, je leo tunaamini shibuda anakubaliana na agenda za Chadema wanazotaka kuziwasilisha kwa Rais? Je waende kukutana na Rais kama fasheni au waende kwa msingi wa mahitaji ya hoja zao.

Anadai atamuunga mkono Diamond, lakini wengine wanaopingana na Diamond anadai wamekosa agenda. Kwanini anaamini kwake kumsapoti diamond ni agenda lakini wengine mmojammoja awapaswi kumpinga diamond? Ni wapi chama kimetoa msimamo wake juu ya bet ya Diamond?

Lakini pia overconfidence inamwondoa kwenye mjadala nakufikia kuona Kama alistahili kuwa mgombea wa Chadema Arusha na si Lema. Je Kama alikuwa na kinyongo juu ya lema kwanini asimwambie?
Anashindwa tu kusema kajitoa chamani [emoji3][emoji3][emoji3]. Atimliwe kama alivyotimliwa mkewe.
 
Msameheni tu kwani Mama ndiye kashika hatamu kwa sasa.
 
Chadema muambiwe mara ngapi?
Huyu na Alibeto dugu moja
Huyu na wasaliti 19 dugu moja
Mnaendelea kumwamini
Atawaanika siku yaja
 
Mkuu umeandiki nini!! Huna elezea hoja ya ku-support mada. Kwa ujumla mtoa mada ameshindwa kabisa kutetea au kujenga hoja yake. Je huyo mkeo ukimkuta chocho hutamuhoji anatafufuta nini huko chocho? Je unajua vitabu vyote vya DINI vinatambua neno TALAKA, kwa nini neno hilo Lipo? TAFAKALI SANA.
Ninatafakari zaidi uandishi wako. Si ulisomea nchi mwenzetu!
 
CCM ili upate viti maalumu unapitia mchakato wa kupigiwa kura. Walau kule kuna demikrasia.
Demokrasia inatoka wapi wakati msibani JK alikiri kuja na jina la marehemu mfukoni?
 
Back
Top Bottom