Ally Bananga: Nina kiapo na mke wangu, nitamlinda kwa gharama ya damu yangu

Ally Bananga: Nina kiapo na mke wangu, nitamlinda kwa gharama ya damu yangu

Good, good! Mwisho wa siku lazima mtu asimame kwenye ukweli. Familia kwanza kabla ya kitu chochote. Huwezi kutelekeza famila halafu eti ukawa mtiifu wa chama. Hata Lissu na Lema walikimbilia nje ya nchi na familia zao! Hawakukimbia na Chadema wala wana Chadema!
mkuu,
umewai sikiliza story ya mke wa Raisi wa kwanza wa Zenji,
apo ndo utaona kua unapo jitoa sana kutetea haki za watu, sometimes familia unaiweka yapili.
Hata Kwa Mandela pia...
 
"Mimi ni mwanachama wa CHADEMA, Suala la wabunge 19 wa viti maalumu ambao Chama chetu kinasema hakiwatambui, mke wangu (Hawa Bananga) pia ni miongoni mwao na katika vitu ambavyo nimekuwa nikijiepusha kuvizungumza ni suala hili kwasababu bado maamuzi yako ndani ya chama,

Kuliweka hili kwa ufupi mimi nitasimama aliposimama mke wangu kwasababu sikufunga naye ndoa CHADEMA, sikufunga naye ndoa mitandaoni nilifunga naye ndoa msikitini, kiapo changu kwake ni kumlinda kwa gharama ya damu yangu....

Lolote lenye udhaifu kwake ni wajibu wangu kulipa uimara, ndio kitu cha thamani ninachomiliki, nitamlinda mama wa watoto wangu

"-Mwanasiasa Ally Bananga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Chanzo: Star TV
Hahaha sasa atabeba zege dadekii
 
Huyu ndugu asingekubali kuliongelea hili au angetafuta namna ya kulikwepa vinginevyo amepotea, hoja yangu ni kwamba kuna mambo yanatakiwa kubaki moyoni au sirini lakini kwa namna alivyoweka bayana ameonesha kabisa kwamba hawa covidd19 wanamwelekeo wa kwenda ccm ili kunusuru maslahi yao kitu ambacho kitapelekea Ally kumuunga mkono na kuunga juhudi pamoja na baadae kubadilika kuwa chlorophyll
 
Nimemsikia Ally Bananga kwenye mahojiano, nadhani amepanic nakuanza vita bila kujua anapambana na nani. Amepambana na Lissu, Lema, Mnyika kwa maana wamekosea sehemu fulani kutokana na tweet zao juu ya kukutana na Rais, Diamond pamoja na wabunge 19.

Anapohojiwa msimamo wake kuhusu wabunge 19 anaeleza kwamba familia Kwanza Katiba baadaye. Najiuliza anaamini hiki ndicho wananchi wanachokihitaji? Leo viongozi wote wa upinzani wakiwaza familia zao watapata muda wakuwaza Katiba mpya?

Anasema wakutane na shibuda Kwanza kabla ya kwenda kuonana na Rais Kama takwa lakukukuna linavyotaka, je leo tunaamini shibuda anakubaliana na agenda za Chadema wanazotaka kuziwasilisha kwa Rais? Je waende kukutana na Rais kama fasheni au waende kwa msingi wa mahitaji ya hoja zao.

Anadai atamuunga mkono Diamond, lakini wengine wanaopingana na Diamond anadai wamekosa agenda. Kwanini anaamini kwake kumsapoti diamond ni agenda lakini wengine mmojammoja awapaswi kumpinga diamond? Ni wapi chama kimetoa msimamo wake juu ya bet ya Diamond?

Lakini pia overconfidence inamwondoa kwenye mjadala nakufikia kuona Kama alistahili kuwa mgombea wa Chadema Arusha na si Lema. Je Kama alikuwa na kinyongo juu ya lema kwanini asimwambie?
Greater thinker
 
Hata asingekwenda kwenye Media kutangaza bado,anawajibu wa kumlinda mkewe!
 
Utaona Ni kwa nini anaunga mkono mke wake kuendelea kuwa mbunge kwa tiketi ya kughushi. Kuna usemi "ushakula nyama ya mtu unakuwa mafia". Huyu alifurahia mshiko wa ubadhirifu.
 
"Mimi ni mwanachama wa CHADEMA, Suala la wabunge 19 wa viti maalumu ambao Chama chetu kinasema hakiwatambui, mke wangu (Hawa Bananga) pia ni miongoni mwao na katika vitu ambavyo nimekuwa nikijiepusha kuvizungumza ni suala hili kwasababu bado maamuzi yako ndani ya chama,

Kuliweka hili kwa ufupi mimi nitasimama aliposimama mke wangu kwasababu sikufunga naye ndoa CHADEMA, sikufunga naye ndoa mitandaoni nilifunga naye ndoa msikitini, kiapo changu kwake ni kumlinda kwa gharama ya damu yangu....

Lolote lenye udhaifu kwake ni wajibu wangu kulipa uimara, ndio kitu cha thamani ninachomiliki, nitamlinda mama wa watoto wangu

"-Mwanasiasa Ally Bananga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Chanzo: Star TV
mkeo akikusalati unamlinda kwa damu yako? Itakua na ww msaliti.
 
Back
Top Bottom