Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
==
Wakati anahutubia Wananchi wa Jimbo la Msalala, Katibu Mkuu wa Umoja wa wazazi jumuiya ya CCM Taifa Ally Hapi alieleza kuwa kuna kipindi Mbowe alitaka kulipua vituo vya mafuta lakini Rais Samia alimsamehe.
Hapi alidokeza kuwa Mbowe alikuwa na nia ovu ya kuleta taharuki nchini kwa kutaka kulipua vituo vya mafuta, mpango ambao ulipeleka kiongozi huyo kukamatwa na kukaa rumande kwa muda, kabla ya Rais kumsamehe na kuacha awe huru.
"Freeman Mbowe alikuwa na kesi ngumu sana ya kutengeneza machafuko kutaka kulipua vituo vya mafuta wananchi wafe. Mashtaka yale yakafutwa, Mbowe akarudi uraiani na wenzao wengine wakarudi uraiani. Rais Samia kwa upendo wake akasema hawa ni watoto wangu. Hebu waacheni warudi uraiani wakafanye siasa. Pamoja na wema wote aliowafanyia huo, leo shukrani ya punda ni mateke"
Ikumbukwe kuwa Freeman alikamatwa na Jeshi la Polis Jijini Mwanza mwaka Julai 2022 alipokuwa akiandaa kongamano la kushinikiza mabadiliko ya katiba mpya nchini humo ambapo mara baada ya kukamatwa alikabiliwa na mashtaka ya ugaidi ikiwemo mauaji ya viongozi.