Pre GE2025 Ally Hapi: Mbowe alitaka kulipua vituo vya mafuta aue wananchi, pamoja na kusamehewa bado wanaeneza uchochezi, hawafai kuongoza nchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu,

==
Wakati anahutubia Wananchi wa Jimbo la Msalala, Katibu Mkuu wa Umoja wa wazazi jumuiya ya CCM Taifa Ally Hapi alieleza kuwa kuna kipindi Mbowe alitaka kulipua vituo vya mafuta lakini Rais Samia alimsamehe.

Hapi alidokeza kuwa Mbowe alikuwa na nia ovu ya kuleta taharuki nchini kwa kutaka kulipua vituo vya mafuta, mpango ambao ulipeleka kiongozi huyo kukamatwa na kukaa rumande kwa muda, kabla ya Rais kumsamehe na kuacha awe huru.

"Freeman Mbowe alikuwa na kesi ngumu sana ya kutengeneza machafuko kutaka kulipua vituo vya mafuta wananchi wafe. Mashtaka yale yakafutwa, Mbowe akarudi uraiani na wenzao wengine wakarudi uraiani. Rais Samia kwa upendo wake akasema hawa ni watoto wangu. Hebu waacheni warudi uraiani wakafanye siasa. Pamoja na wema wote aliowafanyia huo, leo shukrani ya punda ni mateke"

Ikumbukwe kuwa Freeman alikamatwa na Jeshi la Polis Jijini Mwanza mwaka Julai 2022 alipokuwa akiandaa kongamano la kushinikiza mabadiliko ya katiba mpya nchini humo ambapo mara baada ya kukamatwa alikabiliwa na mashtaka ya ugaidi ikiwemo mauaji ya viongozi.

Viongozi TULIONAO HAWAFAI,YAANI WANA USHAIDI ALAFU WANA MSAMEHE MTU WA NAMNA HIYO?
MIMI NIMEMUELEWA HAPPY KWAMBA NA YEYE HAWAHITAJI HAWA VIONGOZI TULIO WAKABIDHI MAMLAKA,HAWAWEZI NA HAWANA UWEZO labda WENYE UWEZO NI HAO WALIO SAMEHEWA.
 
Wakuu,

==
Wakati anahutubia Wananchi wa Jimbo la Msalala, Katibu Mkuu wa Umoja wa wazazi jumuiya ya CCM Taifa Ally Hapi alieleza kuwa kuna kipindi Mbowe alitaka kulipua vituo vya mafuta lakini Rais Samia alimsamehe.

Hapi alidokeza kuwa Mbowe alikuwa na nia ovu ya kuleta taharuki nchini kwa kutaka kulipua vituo vya mafuta, mpango ambao ulipeleka kiongozi huyo kukamatwa na kukaa rumande kwa muda, kabla ya Rais kumsamehe na kuacha awe huru.

"Freeman Mbowe alikuwa na kesi ngumu sana ya kutengeneza machafuko kutaka kulipua vituo vya mafuta wananchi wafe. Mashtaka yale yakafutwa, Mbowe akarudi uraiani na wenzao wengine wakarudi uraiani. Rais Samia kwa upendo wake akasema hawa ni watoto wangu. Hebu waacheni warudi uraiani wakafanye siasa. Pamoja na wema wote aliowafanyia huo, leo shukrani ya punda ni mateke"

Ikumbukwe kuwa Freeman alikamatwa na Jeshi la Polis Jijini Mwanza mwaka Julai 2022 alipokuwa akiandaa kongamano la kushinikiza mabadiliko ya katiba mpya nchini humo ambapo mara baada ya kukamatwa alikabiliwa na mashtaka ya ugaidi ikiwemo mauaji ya viongozi.

Watu kama Hawa bora wasingezaliwa! Wanatia taifa letu aibu sana! Shit!!
 
Back
Top Bottom