Pre GE2025 Ally Hapi: Mbowe alitaka kulipua vituo vya mafuta aue wananchi, pamoja na kusamehewa bado wanaeneza uchochezi, hawafai kuongoza nchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

==
Wakati anahutubia Wananchi wa Jimbo la Msalala, Katibu Mkuu wa Umoja wa wazazi jumuiya ya CCM Taifa Ally Hapi alieleza kuwa kuna kipindi Mbowe alitaka kulipua vituo vya mafuta lakini Rais Samia alimsamehe.

Hapi alidokeza kuwa Mbowe alikuwa na nia ovu ya kuleta taharuki nchini kwa kutaka kulipua vituo vya mafuta, mpango ambao ulipeleka kiongozi huyo kukamatwa na kukaa rumande kwa muda, kabla ya Rais kumsamehe na kuacha awe huru.

"Freeman Mbowe alikuwa na kesi ngumu sana ya kutengeneza machafuko kutaka kulipua vituo vya mafuta wananchi wafe. Mashtaka yale yakafutwa, Mbowe akarudi uraiani na wenzao wengine wakarudi uraiani. Rais Samia kwa upendo wake akasema hawa ni watoto wangu. Hebu waacheni warudi uraiani wakafanye siasa. Pamoja na wema wote aliowafanyia huo, leo shukrani ya punda ni mateke"

Ikumbukwe kuwa Freeman alikamatwa na Jeshi la Polis Jijini Mwanza mwaka Julai 2022 alipokuwa akiandaa kongamano la kushinikiza mabadiliko ya katiba mpya nchini humo ambapo mara baada ya kukamatwa alikabiliwa na mashtaka ya ugaidi ikiwemo mauaji ya viongozi.

Your browser is not able to display this video.

 

Wakuu,​

maendeleo.​

Surat An-Nur (24:15-16) inasema: "Mnapoisema kwa ndimi zenu, na mkaikariri kwa vinywa vyenu kitu msichokijua, na mnakidhania kuwa ni jambo dogo, kumbe mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa."Aya hii inaelezea hatari ya kuzungumza mambo ambayo mtu hana hakika nayo au hakuona mwenyewe, kwa kuwa inaweza kusababisha dhambi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Inaonya dhidi ya kufikiri kwamba kusema jambo bila uhakika ni jambo dogo, kwani linaweza kuwa na madhara makubwa.


Surat Al-Hujurat (49:6) inasema: "Enyi mlioamini! Ikiwa mtu fasiki atakuleteeni habari, basi hakikisheni kwanza, msije mkawaumiza watu kwa ujahili na mkajuta kwa mliyoyatenda."Aya hii inafundisha umuhimu wa kuchunguza habari kabla ya kuzisambaza au kuzifanyia kazi. Mtu hapaswi kueneza habari ambazo hazina ushahidi au uhakika, kwani inaweza kusababisha madhara kwa wengine, jambo ambalo baadaye linaweza kuleta majuto.
 
Kwa hili kama kasema basi Mbowe ana haki ya kwenda Mahakamani. Defamation
 
Noma sana!
 
Afungue kesi else akishtakiwa kwa defamation asije omba huruma
 


Haki nimecheka, yaani siasa za tanzania, tuna safari ndefu sana. Sijuhi kama nchi watu wetu watakombolewaje kifikira.
 
Afungue kesi else akishtakiwa kwa defamation asije omba huruma
Ashitakiwe ki vp wakati hayo hayo yote tunayajuwa!? Hakuna jipya,ni kweli Mbowe alikua Jela na DPP akaondoa kesi bila reason!!
 
Hivi FAM akienda nacho kwa pilato haka katapona kweli!!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…