Pre GE2025 Ally Hapi amesema CHADEMA wasitumie No reform no election kama njia ya kukimbia mapambano, adai mabadiliko Watanzania wameshayaona

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Katibu wa jumuiya ya Wazazi Ally
Hapi amewataka vyama vya upinzani kuacha visingizo vya kukimbia mapambano ya uchaguzi kwani mabadiliko wanayoyataka wapinzani tayari Watanzania wameshayapata.

Ameeleza kuwa mabadiliko hayo yameletwa na Rais Samia, ambapo mabadiliko hayo ni uwepo wa maji na huduma za afya pamoja na mabadiliko mengine.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Hii ndio staili, ya Gen z wa ccm watafuta Teuz. lazima aoneshe kizabizabina chake.
 
Na nyie mkizidiwa kwa hoja msitumie dola na kutekana
Hoja zijibiwe kwa hoja

Ova
 
Katibu wa jumuiya ya Wazazi Ally
Hapi amewataka vyama vya upinzani kuacha visingizo vya kukimbia mapambano ya uchaguzi kwani mabadiliko wanayoyataka wapinzani tayari Watanzania wameshayapata.

Ameeleza kuwa mabadiliko hayo yameletwa na Rais Samia, ambapo mabadiliko hayo ni uwepo wa maji na huduma za afya pamoja na mabadiliko mengine.
View attachment 3240839
Muulize afya gani wakati hospitali hakuna dawa? Muulize Maji gani wakati Dar tu Jiji Kuu la Biashara Ubungo, Kimara na Mbezi hakuna Maji?

Muulizeni twende kwenye uchaguzi wanaoengua wagombea wa Upinzani ili iweje?

Muulizeni twende kwenye uchaguzi ambao Nape alisema unategemea na anayetangaza matokeo na sio kura za Wananchi ili iweje?
 
Hao wakuuliza hayo maswali kaka ndiyo wapo hapo wanashangalia kila wanachoambiwa as if wanakaa mbinguni hizo shida hawazioni
 
Katibu wa jumuiya ya Wazazi Ally
Hapi amewataka vyama vya upinzani kuacha visingizo vya kukimbia mapambano ya uchaguzi kwani mabadiliko wanayoyataka wapinzani tayari Watanzania wameshayapata.

Ameeleza kuwa mabadiliko hayo yameletwa na Rais Samia, ambapo mabadiliko hayo ni uwepo wa maji na huduma za afya pamoja na mabadiliko mengine.
View attachment 3240839
Haya majitu yanakera Sana.
 
Ukiangalia hao wasikilizaji wake, wengi wao wanamshangaa tu.
Kuwe na Tume Huru kwanza ili kura za wananchi ziamue washindi, siyo mambo ya kushinda kwa wizi
 
Hata aibu haoni, kwani CCM anayaweza mapambano, panya akimuona paka ni mbio uvunguni
 
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi, amevitaka vyama vya upinzani kuacha visingizio na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi, akisisitiza kuwa maendeleo yaliyotekelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan yanatosha kuipa CCM ushindi mkubwa.

Akizungumza na wanachama wa CCM wilayani Kiteto wakati wa ziara yake ya siku nne mkoani Manyara, Hapi alisema kuwa maendeleo yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia ni dhahiri na hayahitaji propaganda za kisiasa.

"Tumeshuhudia miradi mikubwa ya maendeleo, kuboreshwa kwa huduma za kijamii, na uimarishaji wa uchumi. Wanaotafuta visingizio vya kukwepa uchaguzi wanapaswa kujitathmini badala ya kulaumu mfumo," alisema.

Aidha, alisisitiza kuwa CCM itaendelea kuaminika kwa Watanzania kutokana na utekelezaji wa llani yake kwa vitendo na kuwataka wanachama wa chama hicho kuwaelimisha wananchi kuhusu mafanikio hayo.
Kauli hiyo inakuja wakati vyama vya upinzani vikiendelea kueleza changamoto za kisiasa nchini, huku baadhi vikidai kuwepo kwa mazingira yasiyo sawa katika uchaguzi.

Hapi amesisitiza kuwa vyama vya upinzani, hususan CHADEMA, visikimbie uchaguzi kwani serikali ya awamu ya sita imefanya kazi kubwa za maendeleo zinazoleta ushindani wa haki.​
 
Katibu wa jumuiya ya Wazazi Ally
Hapi amewataka vyama vya upinzani kuacha visingizo vya kukimbia mapambano ya uchaguzi kwani mabadiliko wanayoyataka wapinzani tayari Watanzania wameshayapata.

Ameeleza kuwa mabadiliko hayo yameletwa na Rais Samia, ambapo mabadiliko hayo ni uwepo wa maji na huduma za afya pamoja na mabadiliko mengine.
View attachment 3240839
Mwaka wa uchaguzi mkuu wa nchi unafanya uchaguzi mkuu wa chama ....

Kabla ya mabadiliko ya katiba ya nchi yaanze kwanza mabadiliko ya katiba ya CHADEMA....ndugu.Mnyika ameelezea hayo pia .....

Wasikimbie mapambano kwani wenzao walishajipanga vyema tu......

#Hapa hakuna kukimbia !
 
Back
Top Bottom