Ally Kamwe ametuelewa bado Ahmed Ally

Ally Kamwe ametuelewa bado Ahmed Ally

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Simba na Yanga ni timu kubwa zenye wafuasi wengi wenye hadhi tofautitofauti, zinahitaji wasemaji mahiri sio wasema chochote wanachojisikia wao hata kama hakina maana wala uhalisia.

Hata kama ni utani lakini unawezaje kusema Yanga woooote hawana akili isipokuwa watu wawili tu kwenye timu ambayo ina wafuasi wenye madaraja mbalimbali ya elimu, viongozi, umri, uchumi na kiroho?

Ally Kamwe alikuwa na tabia ya kuwapa baadhi ya wachezaji wa timu hiyohiyo sifa nyingi sana na wakati mwingine sifa zisizo wastahili ambazo ziliwasababishia kukamiwa uwanjani na kuumizwa au kuwavunja moyo wachezaji wengine ndani ya kikosi.

Sio vyema baba kuwatenga watoto wake hadharani kuwa mwenzenu huyu ni mzuri kuliko nyie, ni mwaminifu kuliko nyie badala yake mwache Mchezaji anaefanya vizuri asifiwe na mashabiki wenyewe au wachezaji wenzake.

Kutoa sifa na matarajio yanayokinzana na tabia ya mpira na uwezo wa Mungu nayo ni kuwakosea mashabiki heshima hasa pale matokeo yatakapokwenda tofauti na majigambo na uropokaji wako. Ally kapunguza kama sio kuacha kabisa.

Ahmed Ally bado anazo hizo, anadharaulika mitaani na kumuuona mropokaji tu. Hivi ni kweli Onana ni Ronaldo mtupu? Hivi ni kweli Che Malone ni ukuta wa Yeriko? hivi ni kweli Miquison amerudi kwenye kiwango chake kilichowafanya Al-Ahly wamsajili?

Hivi ni kweli Simba ni lazima izifunge timu ndogo zote Tanzania kila zikikutana? Ni uropokaji au uhalisia?
 
Simba na Yanga ni timu kubwa zenye wafuasi wengi wenye hadhi tofautitofauti, zinahitaji wasemaji mahiri sio wasema chochote wanachojisikia wao hata kama hakina maana wala uhalisia. Hata kama ni utani lakini unawezaje kusema Yanga woooote hawana akili isipokuwa watu wawili tu kwenye timu ambayo ina wafuasi wenye madaraja mbalimbali ya elimu, viongozi, umri, uchumi na kiroho?

Ally Kamwe alikuwa na tabia ya kuwapa baadhi ya wachezaji wa timu hiyohiyo sifa nyingi sana na wakati mwingine sifa zisizo wastahili ambazo ziliwasababishia kukamiwa uwanjani na kuumizwa au kuwavunja moyo wachezaji wengine ndani ya kikosi. Sio vyema baba kuwatenga watoto wake hadharani kuwa mwenzenu huyu ni mzuri kuliko nyie, ni mwaminifu kuliko nyie badala yake mwache Mchezaji anaefanya vizuri asifiwe na mashabiki wenyewe au wachezaji wenzake. Kutoa sifa na matarajio yanayokinzana na tabia ya mpira na uwezo wa Mungu nayo ni kuwakosea mashabiki heshima hasa pale matokeo yatakapokwenda tofauti na majigambo na uropokaji wako. Ally kapunguza kama sio kuacha kabisa.

Ahmed Ally bado anazo hizo, anadharaulika mitaani na kumuuona mropokaji tu. Hivi ni kweli Onana ni Ronaldo mtupu? hivi ni kweli Che malone ni ukuta wa Yeriko? hivi ni kweli Miquison amerudi kwenye kiwango chake kilichowafanya Al-Ahly wamsajili? ?: Hivi ni kweli simba ni lazima izifunge timu ndogo zote Tanzania kila zikikutana? Ni uropokaji au uhalisia?
Bandiko refu, anayesimangwa ni mfupi, kimo cha msimangaji sijui ni futi ngapi 😁😁
 
Hivi vyeo ni vya kipuuzi naonaga wanaongea ujinga tu, hivi kweli mtu anakuambia timu za ufaransa zinamgombania onana alafu kesho tena unaendelea kumsikiliza
Vijana wamepewa kusemea timu ambazo hata Marais, mawaziri wakuu, maprofesa, Mamajor Generals, magenerali, masheikh, mufti, maaskofu, wafanyabiashara, nk wanashabikia humohumo, wewe utawezaje kujiropokea tu kama vile unaongea na wahuni wenzako? watoto wenzako? wanahabari wenzako tu?. Mtu anasema eti Yanga kuna watu wawili tu wenye akili hiyo ni sawa? ni uhalisia au uropokaji tu?. Huwezi kushangaa kusikia kuwa mropokaji kama huyu kafungiwa miaka 20 asijihusishe na mpira. Nitafanya utafiti kujiridhisha kama timu kubwa za ulaya pia zina wasemaji wa aina hii ambao hawajafungwa jela. Kumfananisha Onana na Ronaldo ni kumdhihaki na kumdhlilisha mchezaji mbele za watu, anaweza kufanya hivyo shabiki lakini sio kiongozi mkubwa wa timu.
 
Hata kama ni utani lakini unawezaje kusema Yanga woooote hawana akili isipokuwa watu wawili tu kwenye timu ambayo ina wafuasi wenye madaraja mbalimbali ya elimu, viongozi, umri, uchumi na kiroho?
Hapo alimnukuu yule mzungu wa GSM aliposema wenye akili pale UTO ni wawili tu
 
Hapo alimnukuu yule mzungu wa GSM aliposema wenye akili pale UTO ni wawili tu
Kuna wakati wasemaji wa aina hii sijuti wakifungiwa hata milele ikibidi ila kwa haki.

Kisa cha Nabii Yusuf hata kwenda kutumbukizwa kisimani na ndugu zake kilisababishwa na mzazi wake kumsifu mbele ya ndugu zake. Ally Kamwe na wasemaji wengine waache kuwasifu baadhi ya wachezaji na kuwaacha wengine, kwani mchezaji mzuri atatangazwa na kazi zake ndani na nje ya kikosi.
 
Back
Top Bottom